MAKONDA ATANGAZA NEEMA: AHAIDI USHIRIKIANO KWA WANA ARUSHA

Egidia Vedasto

Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha Paul Makonda amewataka wananchi walio tayari, kumshirikisha katika mipango yao ya Maendeleo ili kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ya Uchumi katika Mkoa wa Arusha. 

Akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa(AICC) Jijini Arusha, amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa wananchi hata kwa namna ya kupata fedha ili kufanya miradi itakayoleta maendeleo haraka. 

Aidha ameongeza kuwa, si vema wananchi wazidi kujenga vyumba vya biashara (flemu) na badala yake waangalie namna ya kuongeza vyumba vya kulala wageni ili kuendana na ongezeko la wageni wanaoingia Jijini na wageni watarajiwa wa mwaka 2027, inapotarajiwa kufanyika mashindano ya AFCON. 

"Mpaka sasa tuna upungufu mkubwa sana wa nyumba za kulala wageni, naona hii inasababishwa na watu wengi kukimbilia kujenga vyumba vya biashara badala ya kuwekeza katika nyumba za kulala wageni hatua ambayo naamini itazidi kukuza uchumi tena kwa haraka" Amesema Makonda. 

>Hata hivyo kwa kutambua upungufu wa nyumba za kulala wageni amewakumbusha wananchi kuchangamkia fulsa, Kwa kukaa na Mkuu wa Mkoa ili kubadilishana mawazo na mbinu ya kukuza Uchumi. 

"Unaweza kuona mpaka sasa vyumba vyote vya kulala wageni vimejaa na watu bado wanahitaji kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi inayotarajiwa kufanyika jijini hapa, hii inaonyesha ni kiasi gani wawekezaji waangalie mahali pa kuwekeza, Ndio maana nimesema niko tayari kutoa ushirikiano wa kina kuhakikisha tunaibadilisha Arusha yetu inakuwa ya Dola" ameeleza Makonda

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post