Ijue Historia ya Wajita na asili yao

Ungana na Faida Potea kujua kabila la wajita.

Wajita ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kijita. Wajita wana muingiliano mkubwa na makabila kama Waha, Wahaya, Wanyankole, Wanyoro, Watoro, Wakerewe, Wahangaza, Wanyambo, Wazinza, Wakara, Wakabwa, Waruri, Wakwaya na kadhalika. Kulingana na historia yao wengi waweza kuitana wajomba. 

Bila kusahau Wajaluo ambao ni watani wao. Wajita nao wana koo nyingi sana kama Rusori, Bahitira, Bajigamba, Batimba na wengineo. 


Wajita ni watu wachapakazi sana na wasiopenda dhihaka kwenye kazi, wenye msimamo sana na wapole, ila wakali sana wanapoonewa, wenye kupenda utani.


 Historia Inasemekana makabila mengi ya mkoani Mara si Wabantu asilia lakini walipokuja mkoani Mara wengine walichagua kuzungumza lugha ya Kisuguti na lugha nyingine za Mara.


Inawezekana Wajita wengi wana asili toka Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan kaskazini kama Wanubi na pia Niger kama Wahausa na Nigeria kama Waigbo. 


Kati ya vijiji vingi vya Wajita utavikuta pia Rwanda, Uganda, Burundi. Kati ya vijiji hivyo mfano ni Rusori, Buringa na vinginevyo vingi tu. Wajita wengi nao wana koo zao ambao hata wakienda Rwanda, Uganda, Niger, Burundi ni rahisi kutambua koo zao kulingana na miiko yao. 


Kama jamii zingine zozote zilizoweza tambua ndugu zao kutokana na miiko, mfano ya nyama ama vyakula vingine. Mfano: Wajita wa koo za Rusori wengi kuna samaki hawali, ila kulingana na mazingira ya siku hizi watu kutoelewa wanajikuta wakila samaki. Mila hizo pia ziko kwa Wanyoro wengi, Watoro na Wanyambo.


 Wajita wengine hawawezi kuua chatu na ni mwiko kabisa kama vile kwa Wahausa, Waigbo, na pia wengine wanaheshimu sana chura kama ilivyo kwa koo nyingine nchini Rwanda. Wajita wenye asili ya Kibantu ni wengi sana na wanatokea katika koo za Bahitira. 

Mfano Waruri wengi ni Wabantu na wanatokea Bururi na ni kabila ambalo pia liko Uganda. Pia wapo ambao wana asili ya Kush. Mfano: inaaminika Wajita wa kwanza kufika Musoma na wanaojiita Original ni wale wenye asili ya Warusori; mpaka sasa wao ni weupe na warefu sana, wapo na pua zao za kuchongoka. Yasemekana hao si Wabantu,

wana asili ya Kinubi na Ethiopia na wengine pia wanatokea Bunyoro na wengine wakaenda Rwanda na Burundi. Wajita wengi wenye asili ya Banyoro ni warefu

sana, ingawa wengine ni weusi siku hizi kutokana na mchanganiko. Wenye asili ya Nubia na hao Banyoro zamani walikuwa kama Waarabu kwa mbali, ambao wengi wasemekana ni hao Warusori.

Mimi Faida potea kazi yangu kukumbushana mambo kama haya

1 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. Mungu wangu... Kwa nini haya yanatokea...

    Tufanyeje sasa jamani...

    Mauaji ya kikatili...

    ReplyDelete
Previous Post Next Post