MWANDISHI JAMAL AHMAD KHASHOGGI NA UTATA WA KIFO CHAKE.

 MWANDISHI JAMAL AHMAD KHASHOGGI NA UTATA WA KIFO CHAKE.


Anaitwa Jammal Ahmad Khashoggi ,alizaliwa mji wa madina nchini Saudi Arabia tarehe 13 octoba 1958 na amekufa tarehe tar 2 octoba 2018,Istanbul ,Uturuki,Baba yake ni Muhammad khashoggi alikuwa mturuki ila alioa mwanamke wa Saudi Arabia.alikuwa daktar wa viungo wa mfalme wa Saudi Arabia kipindi hiko cha zamani.


Khashoggi alipata elimu yake ya msingi na sekondari Saudi Arabia ,na Shahada yake (bachelor degree)aliipatia chuo cha Indian state university nchini Marekani BBA (Business Administration) na  uandishi wa Habari. 1982.


Alirejea nyumbani Saudi Arabia 1983-1984 kuhudumu katika kampuni  kama meneja wa kikanda wa TIHAMA BOOKSTORES (kampuni inayojihusisha na uchapishaji,usambazaji vitabu,matangazo na masuala ya elimu)mwaka 1985-1987 akateuliwa kama meneja msaidizi wa Gazeti la OKAZ saud Arabia.Baadaye katika Gazeti la Saudi Arabia ,vyombo vya habari kama Asharq Al-Awsat ,Al-Majalla,Al-Muslimoon,pia na alipata kuwa mhariri Mkuu katika vyombo hivi.


Akaendelea miaka ya 1991 hadi 1999 alijikita kuandika juu ya vita ya Soviet na Afghanistan, pia akandika juu sudani,Algeria na Kuwait.


Ndiye Muandishi aliyekuwa aki-Cover interview yeye na Osama bin Laden  ,alikuwa akimfuata kumuhoji katika milima ya Spin Ghar mountain nchini Afghanistan ,katika mapango ya Torabora ,pia alikuwa akiajiriwa na kitengo cha intelligence cha Saudi Arabia ,pia kilimpa kazi ya kumshawishi Osama Biladen kuacha Uadui na watafute suluhu na Familia ya kifalme ya Saudi Arabia.


Khashoggi aliepuka ukaribu na Osama baada ya shambulio la September 11,Alipainga sana na alilaani sababu imepelekea watu kufa ,alilaani watoto wa Saudi kutumiwa na Osama ,akisema.


"The most pressing issue now is to ensure that our children can never be influenced by extremist ideas like those 15 Saudis who were misled into hijacking four planes that fine September day"


2003 aliajiriwa Gazeti la Al-watan kama mhariri Mkuu ila baada miezi 2,alifukuzwa kazi na wizara ya habar,tukumbuke kuwa habar nyingi za khashoggi zilikuwa ni za kukosoa kuleta mabadiliko tutaona mbele ! Baada ya kufukuzwa kazi.


Aliamua kwenda Uingereza kuishi akawa msaidizi na mshauri  masuala ya Habari  wa Prince Turk Al-Faisal Bin Abdul Azizi ambaye mwanzo alikuwa Mkuu wa kitengo cha usalama wa Saudi kabla ya kuwa Balozi wa Saudi nchini Marekani.


2007,alirejeshwa kazi nchini Saudi Arabia ,katika Gazeti lilelile Al-watan kwa mara ya pili ,haikupita Muda pia ilitangazwa kuwa amejiuzulu ila ukweli aliachishwa kwa nguvu baada ya kuendelea uandishi wake wa kukosoa sheria za Kali katika utawala wa kifalme.


Aliamua kufungua Gazeti la kujitegemea nje ya nchi ,sababu sheria za Saudi haziruhusu independent media ,hivyo alifungulia Nchini Bahrain akisapotiwa na Tajiri ,mfanyabiashara mkubwa ,muekezaji Alwaleed Bin Talal(umkumbuke huyu baadaye).Bahrain muda walifungia Gazeti hilo.


Khashoggi aliweka nguvu sana katika vyombo kadhaa vya Saudi Arabia na Vyombo vya habar vya kimataifa kama Aljazeera,BBC,Dubai TV,Al-Arabya TV,na vyombo vya Emirates kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa (political commentator),muhabarishaji,na muandishi mchunguzi kipindi cha 2012 -2016.


Katika kipindi chote hiki Khashoggi alikuwa akipinga kupitia uwandishi wake kukosoa sheria kali dhidi ya uhuru wa watu na haki za Binadamu, moja ni kuhusu wanawake kutokuruhusiwa kuendesha Gari hii ilipelekea wanamama kama Aziza al -yousouf ,Eman Al-Nafjan ,Loujain al-Hathloul ambao walikutwa wakiendesha Gari mji Mkuu Riyadh ,hawa ni wana harakati waliokuwa wakipinga Sheria hizo ,wamekuwa wakifungwa ila Khashoggi amekuwa akikosoa vitendo hivyo.


Tarehe 10,Dec,2016 baada ya ushindi Wa Donald Trump ,Saudi Arabia likuwa ikisherekea ushindi Wa Trump ila Khashoggi alikosoa vikali kupitia Twitter,na Washington post article,juu ya ushindi wa trump ambaye ni Rafiki wa saudi akisema.


"When his advisers show him the map, will he realize supporting Putin means supporting the Iranian agenda? And this is what Saudi Arabia is concerned about, to stop Iranian hegemony,” he told reporter Liz Sly.


Hii ilimuudhi sana Prince Mohammad bin Salman , Khashoggi akafungiwa na serikali ya Saudi kuonekana kwenye TV ,kuripoti habari,kuandika na pia hata kuhudhuria mikutano.


Khashoggi aliamua kuondoka kuelekea Marekani mnamo June,2017 na kuanza kuandikia katika Gazeti la Washington post.akaendelea kuikosoa vikali Saudi Arabia na utawala wa Prince Mohammed, pia alikosoa dhidi ya Saudi Arabia led Blockade against Qatar , vizuizi vya usafiri wa Anga ,majini na nchi kavu ambapo Saudi Arabia ilishawishi nchi zingine kama Libya,Egypt,Senegal,Emirates,Jordan na Comoros kuweka vizuiz dhidi ya Qatar eti Qatar anasapoti Ugaidi (Terrorism) Khashoggi alipinga kabisa vizuizi  hivyo.


Pia Khashoggi aliendelea kupinga kukamatwa kwa mwanamke mwanaharakati  Loujain Al Hathloul(muasisi wa campaign ya kupinga wanawake kutoendesha gari) na ile sheria ya kibali kutoka kwa mwanaume kabla kufanya Jambo lolote waliopinga kupitia Ant-Male Guardship campaign) na baadaye kukamatwa  kwa mashtaka kuwa ana  pambana dhidi ya serikali ya kifalme.


Khashoggi aliendelea kupinga juu ya njia ya kupambana na ufisadi ya Saudi Arabia inaitwa Ant-Corruption crackdown) ambapo wafanyabiashara wengi,matajiri,wawekezaji walikatwa akiwemo Alwaleed Bin Talal ,walikamatwa na kuwekwa katika hotel ya Ritz Carlten Hotel mjini Riyadh wakipewa kosa la utakatishaji fedha,Ufisadi na wakapewa masharti wajichange kurudisha kiasi cha $100bil serikalini ,kwamba hiyo ni hela ya serikali,Khashoggi alikuwa akiandika sana kukosoa na kupinga hatua hii.


Aliendelea kutetea uhuru wa kuongea na kupinga ukandamizwaji wa Uhuru wa kuongea


"Kiongozi wa Saudi Arabia Crown prince Mohammed Bin Salman  anafanya mageuzi ya kiuchumi nchini na huku hakuna uhuru wa watu kuhoji ,wala kukosoa hakika hata ona makosa na kasoro katika mageuzi hayo anayo yafanya,huwezi kuwa na mabadiliko ya kiuchumi bila kuwa na mabadiliko ya kisiasa " katika mahojiano ,Jamal Khashoggi  akimueleza moja ya mchumi.


"The crown prince is engaging in a major economic transformation. And since there is no one to debate it, he will not see the (mistakes) of these transformations ,you can not have an economic reforms unless you have the  political reforms Jamal Khashoggi told the Economist.


Aliendelea kukosoa kupitia gazet la Washington post (Wapo),Juu ya uadua kati ya Saudi Arabia na Yemen ,hii ni nakala yake ya sept.2018 ,"Saudi Arabia's crown prince must Restore dignity to his country-by ending Yemen's cruel war to avoid people from death and suffering."kiongoz wa Saudi lazima alinde heshima na utu wa nchi yake kwa kumaliza vita ya kikatili na Yemen kuepuka Vifo vya watu na mateso.


Pia aliendelea kuandika Nakala  Washington post  akaandika


"SAUD ARABIA WASN'T ALWAYS THIS REPRESSIVE ,NOW IT IS UNBEARABLE" (saudi haijawahi kuwa Taifa la kugandamizaji na udikteta namna kama ilivyosasa hii sio ya kuvumilia "


Alafu akaatweet pia akisema ,sijisikii vizuri kuandika hii nakala au habari katika Gazeti la nje (Washington post )ila ukimya hauwezi kusaidia nchi yangu au waliofungwa ,katika Twitter Governor wa jimbo la mecca , Prince Khaleed Al-Saud  akamjibu kwa kucoment "our guided leadership doesnot need advice from you and your likes" kwa ufupi alijibu uongozi wetu hauhitaji ushauri kutoka kwako.


Kipindi ambacho Jamal Khashoggi alipokuwa marekani alikuwa akihudhuria mikutano nchi mbali mbali,nchini uturuki katika mkutano alipata kuonana na mwanamke msomi miaka 36 ,PHD candidate, katika chuo cha Istanbul anaitwa Hatice Cengiz walikutana may katika mji huo nchini uturuki .wakapanga kuoana .


Hivyo Khashoggi tar 2 October alitembelea ubalozi wa nchi yake ya Saudi Arabia nchini Uturuki (Istanbul )ili kuweza kupata paperwork inayomruhusu yeye Kumuoa Hatice Cengiz,Tar 02 October 2018 aliingia ubalozi wa Saudi Arabia (saudi Arabia Consulate )  nchini uturuki mjini Istanbul .


Baadaye taarifa zikatoka kuwa haonekani ,taarifa zikawa zinatoka kuwa mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi wa Saudi Arabia nchini uturuki na vyanzo vinasema hakutoka tena ,ubishani ukawa mkubwa saana siku za mwanzo baada ya kupotea kwake maafisa wa Saud Arabia wanasema alitoka salama salmini .


Ila maafisa usalama serikali ya uturuki waliendelea kupinga kuwa wana CCTV kamera inayoonesha kuwa alipoingia hakutoka tena,hii inafuatiwa na pressure kubwa kimataifa kutaka Saudi Arabia iseme ukweli  .Baada ya wiki 2 kuisha juzi taarifa rasmi kutoka kwa Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia ,Adel -Jubeir alijitokeza kwa vyombo vya habari kusema kuwa ni kweli Jamal Khashoggi aliuwawa katika jengo la ubalozi wa Saudi huko uturuki ,Istanbul ila kulitokea ugomvi wa ngumi "Fistfights" kati ya maafisa na Jamal Khashoggi ,wakasema prince Mohammed Bin Salman ,hajawahi kuagiza wala hakuwa na taarifa juu ya kifo chake ,


Hivyo wakadai wamewashikilia maafisa 18 wanaodhaniwa kuhusika na kifo na wengine tayar wamefukuzwa kazi ,pia prince Mohammed kuwa ameumia saana juu ya kifo hiko ndio Maana amemualika mtoto wa Khashoggi,Salah kumpa rambirambi yake.Na kweli hawana taarifa wapi  mwili wa Khashoggi ulipo.


Oohhh,Taarifa hii ikaibuwa Maswali mengi ,huku ma afisa usalama wa uturuki wakisema taarifa ya Saudi Arabia sio ya ukweli kwani wameanza danganya tangu mwanzo wa tukio ,kuwa alitoka salama wakasema wana audio na video ikionesha kuwa ni maafisa wa Saudi ndio walimuawa kwa kumtesa ,baada ya Khashoggi kukataa kulazimishwa kurudi Saudi Arabia ,taarifa wanasema ma Afisa hao ni 15 walifika kutoka Saud Arabia(airport reports) wakitumwa na Deputy Head of General intelligence presidency Ahmed Al-Asir kutuma maafisa 15 kumkamata Khashoggi ila walimuua mmoja akavaa nguo za Khashoggi kuonesha kuwa alitoka na mwili wana uhakika umetupwa katika msitu wa Belgrade ,mji wa Yalova na wataupata ukweli utadhihirika.


Wakati huo huo Rais Wa uturuki ,Erdogan akisema kuwa wanafuta haki ,na suala hili litafichuliwa hapo jumanne atakaposoma taarifa hiyo bungeni.


Erdo─čan told a rally in Istanbul: “We are looking for justice here and this will be revealed … not through some ordinary steps but in all its naked truth on Tuesday.”


Upande wa France,Germany, Canada, na uingereza wameungana pamoja(Joint statement) kuhoji juu ya credibility ya taarifa ya Saudi Arabia ,na kusema wanataka kufahamu ukweli mzima kwani wanasubiri taarifa kamili za uchunguzi kutoka Uturuki na sio saud Arabia.


Wanasubiri taarifa kamili ili kuchukua hatua dhidi ya Saudi Arabia,hasa katika kuwawekea vikwazo.


Upande wa Rais Donald Trump baada ya kupata mashinikizo kutoka Congress kuwa kuna haja ya kuweka vikwazo dhidi ya  Saudi hasa kukata mahusiano ya uuzaji silaha kwa Saudi,Trump ametoa kauli yake hivi karibuni kuwa anaishutumu Saudi Arabia kwa kutoa taarifa za uongo mwanzo wa tukio hili. Lakini akionesha kutoamini kama agizo la mauwaji lilitolewa na Prince Mohammed, akasema hakuna anayefahamu juu ya hili ,na hata mwili wa khashoggi hakuna anayejua ulipo ,


"Nobody seems to know. Somebody knows, but nobody of the various investigation groups at this moment know"


Hata kukata mahusiano ya biashara ya silaha ,Trump alisema kuwa watakao umia zaidi ni US kuliko Saudi hivyo wataweka vikwazo vingine na kukemea hili lisijirudie ila sio vikwazo vya uuzaji silaha.


Taarifa kamili zinasubiriwa kutoka kwa serikali ya uturuki juu ya kifo cha Khashoggi na pia upatikanaji wa Mwili wake.huku ndugu na jamaa wakihitaji mwili wa Khashoggi ili wakafanye maziko na msiba .hali bado ni tete,tuendelee kufuatilia suala hili kwa ukaribu zaidi.


KUKAMATWA KWA GARI LA UBALOZI.


 Magari ambayo yana plate namba za light Blue ni magari ya ubalozi ambayo yana maandishi meupe katika plate namba ya light blue ,magari haya plate namba zake huanzia na ufupisho wa UN(united nations),CD (Diplomatic corps) au CC (Consular corps ).


Sasa tutajikita juu ya Consular Corps ,(CC) hawa ni wafanyakazi wa ubalozi katika nchi fulani wakiwakilisha nchi yao.(concerning the staff, estates and work of a consulate). 


Sasa huko Uturuki CCTV zimeendelea kufanya kazi kwa kuonesha Gari la maafisa wa ubalozi wa Saudi Arabia ,ambalo limetelekezwa na linahisiwa ndio lilikuwa la wahusika maafisa wa ubalozi waliofanya tukio hilo Gari hilo plate namba zake ni 34 CC 1736 .taarifa imetoka tar 22 October ,Jana ,jumatatu  ikionesha Gari hili lililotelekezwa.


Hili ni jambo ambalo linasemwa kuwa uturuki wanafanya kazi zao kwa taaluma Kwa kutanguliza utu wa binadamu mbele ndio maana maafisa na hata Rais wao ameampa kuonesha ukweli wote ili kulinda Utu wa binadamu na kuwa tayari hata kuingia mgogoro wa kidiplomasia na Saudi Arabia ila sio kufumbia macho suala hili hata kama Jamal Khashoggi hakuwa RAIA wao ila wanadai HUMAN RIGHTS IS UNIVERSAL ! inainatakiwa kuheshimiwa Dunia nzima na kila mtu.


Huku Afrika kwetu nchi nyingi maafisa wangeweka taaluma zao chini  na kuungana na ubalozi kudanganya  ili kuhofia mahusiano yao ya kidiplomasia hata kama angekuwa ni RAIA wao ndio amekufa,sababu wanaona uhai wa mtu mmoja sio Muhimu kuharibu diplomasia na nchi hiyo .


Maafisa wa Uturuki na Rais wao sio kwamba wana teknolojia ya kutosha hata ila wana utu,na uheshimu uhai wa mtu ,na hufanya kazi kwa kufuata taaluma zao.


Wangeweza sema ni kweli Khashoggi aliondoka salama ,wakakaa kimya ! na wakasema CCTV hazioneshi na hazipo .ingetosha sasa Khashoggi hata hivyo hakuwa RAIA wao.


ALIYOYAONGEA RAIS WA UTURUKI ,Recep  Tayyip  Erdogan JUU YA MAUWAJI YA Jamal Khashoggi.TAR 23 ,October.


siku ya jumanne ,Tar 23 Rais wa Uturuki amehutubia huko mjini Ankara ,Uturuki na kufafanua juu ya mauwaji ya muandishi wa Saudi Jamal Khashoggi huko Istanbul.


Alianza kwa kusema kuwa mauwaji ya Khashoggi yalikuwa sio bahati mbaya ,yalikuwa mauwaji ya kupangwa na ya kikatili. 


Akaendelea kuzungumzia juu ya taarifa ya Saudi kuwa Jamal alikufa wakati wakigombana na ma afisa usalama wa Jumba la  Ubalozi akisema sio  kweli  ,akaongezea hata Uchunguzi uliofanywa na Saudi kupelekea kukiri aliuwawa na watu 18 kushikiliwa bado uchunguzi huo haujafikia matarajio ya juu kufahamu wote waliohusika katika mzunguko huo.


"Saudi investigation, which has resulted in the arrests of 18 people so far, had not reached high enough into the kingdom’s ruling circles"


Akaendelea kusema kuwa haita saidia umma kutosheka na hatua hizo kwa kuchukulia hatua hao mafisa usalama na mafisa wa intelejensia 18 tuu,kuficha jambo hili itapelekea kupotea kwa hali ya uwepo wa utu na ubinadamu.


“It will not satisfy the public by just pinning this kind of matter on a few security and intelligence officers,” he said. “Covering up this kind of savagery will hurt the conscience of all humanity.”


Saudi Arabia imechukua hatua Muhimu kwa kukubali mauwaji haya kuwa yalifanyika,hivyo basi tunatarajia  wawaweke wazi wote waliohusika juu ya jambo hili sababu tuna taarifa kuwa mauwaji haya yamepangwa.


"Saudi Arabia took an important step by accepting the murder. After this, we expect them to reveal those responsible for this matter. We have information that the murder is not instant, but planned,”


Akaendelea kusema kwa kuomba kufanyike " Extradition " kwa watuhumiwa wote waliohusika wakabidhiwe Kwa mamlaka ya Uturuki wa weze kushtakiwa uturuki kwa makosa yao na sio saudi .


Aliendelea sema kuwa mafisa 15 walitumwa kuja Istanbul walikuwa wamejiandaa kikamilifu kutenda mauwaji ya Khashoggi,


"The team of Saud  agents who were dispatched to Istanbul had carefully prepared for Khashoggi's death" 


Anasema Tar 28 ,September Ijumaa Khashoggi alitembelea Ubalozi wa Saudi hapo Istanbul ili kupata documents juu ya ndoa yake na mchumba wake Hatice Cengiz ,akaambiwa arudi tar 2 October ,hivyo kabla ya tar hiyo siku tatu mipango ikaanza kusukwa juu ya mauwaji yake .ambapo tar 1 October timu ya maafisa 15 kutoka saudi walifika Istanbul ,ambapo kuna timu moja ilitembelea sehemu ya msitu kwa kutambua aina ya eneo na kujipanga kwa mpango wa mauwaji na waliondoka Istanbul siku ambayo Khashoggi aliuwawa.


"Planning and the work of a road map starts here,” the president said. Beginning three days later, on Oct. 1, teams of Saudi agents begin arriving in Istanbul, with one team visiting wooded areas in and around Istanbul for reconnaissance"


Ambapo inasemekana ndio sehemu ambayo mwili ulitupwa hapo ,ingawa bado wanaendea na uchunguzi kutafuta mwili  ulipo.


kati ya maafisa 18 waliokamatwa na Saud mafisa tuu 15 ndio waliotambuliwa na maafisa wa uturuki kuwa walihusika na mauwaji ambapo waliingia  Istanbul tar 1 octoba na kuondoka siku Khashoggi alipouwawa,


"Among 18 arrested by saud  only 15 have been identified by Turkish police as numbers of hit squad who flew in and out of in Istanbul the same day Khashoggi killed"


Anaendelea sema baada ya mafisa hawa kufika Istanbul ,katika ubalozi huo hard disc ya camera zilizokuwepo ziliondolewa katika ubalozi huo,na Team ya watu hao walihusika walikuwa watu wa  intelenjensia ,ma afisa usalama na watu wa utambuzi (Forensic workers).


Khashoggi aliingia ubalozini hapo saa saba na dakika 14 mchana (7:14) October 2 ,akiwa na mchumba wake Hatice Cengiz akimsubir ndani ya Gari nje ,baada ya muda mrefu Khashoggi kutotokea ,Mchumba wake haraka alitoa taarifa kwa mamlaka ya Uturuki na uchunguzi ukaanza haraka.


Rais wa Uturuki kwa kuonesha uhusika wa Saud,aliendelea kuuliza maswali haya! 


1.kwanini siku 3  kabla ya tukio October 2,watu 15 kutoka saudi waliingia ,Istanbul tar 28 sept. na kutoka siku ambayo Khashoggi aliuwawa?


2.Nani aliyewaagiza hawa watu au walitoa agizo hilo kutoka kwa nani?


3.kwanini ubalozi wa saud ulifungwa haraka haukuwa wazi kutoa huduma hadi siku uchunguzi unaanza,?


4.ikiwa mauwaji yapo wazi yalifanyika na kila kitu kipo wazi kwanini taarifa ya saudi ya mwanzo juu ya mauwaji haya walikana na kutoa maelezo yasio endana ! 


5.kwanini mwili wa Khashoggi haujapatikana hadi sasa ? 


Akaendelea kusisitiza watuhumiwa wote wakabidhiwe Uturuki washtakiwe uturuki.na hawezi kufichuo audio recordings kwasasa  zilizopatikana muda baada ya Khashoggi kuuwawa 


Akapendekeza Saudi ifanye uchunguzi huru ,ambao watakao fanya uchunguzi huo wasiwe na mahusiano na wanaohisiwa kuhusika katika mauwaji hayo.


MUENDELEZO WA HABARI JUU YA MAUWAJI YA MWANDISHI JAMAL KHASHOGGI.


Tuliishia baada ya Rais wa Uturuki kufanya mkutano J.nne na kuelezea tukio lote kinaga ubaga akishutumu kuwa kifo cha Jamal sio cha bahati mbaya ila kilipangwa,na akaongezea hawezi kutoa wazi recordings zinazothibitisha wazi juu ya mauwaji hayo hadi maswali aliyoyaibua yajibiwe na Saudi Arabia,akaongezea kutaka uchunguzi huru ufanyike Saudi ambao utahusisha maafisa kutoka nchi nyingine sio ndani ya Saudi,akaongeza kuwaomba wote waliohusika wakashtakiwe Uturuki na sio Saudi Arabia.


Siku hiyo hiyo nchini Saudi Arabia uongozi wa kifalme wa Saudi ulimualika Mtoto mkubwa wa Mwandishi huyo aitwaye Salah Bin Jamal Khashoggi kwenda kuonana na prince ,Mohammed Bin Salman,ili atoe Rambirambi zake kwa familia ya mwandishi huyo,wakati wakisalimiana prince alitamka "MAY GOD HAVE MERCY ON HIM" Mungu ambariki huko alipo.


Jambo hili lilizua taharuki dhidi ya mtoto huyo ,baada ya serikali ya Saudi kusambaza picha za mtoto huyo akishikana mkono (Shake hand) na Prince huyo wa Saudi ,wengi wakahoji kwanini Mtoto wa Jamal amekubali kushikana mkono na Kiongozi anayedhaniwa ulimwenguni kuuwa Baba yake,wengine wakisema atakuwa amelazimishwa na serikali hiyo sababu hata ukiangalia picha iliyopigwa mtoto anaonekana kuwa na kitu katika moyo wake.


Pia inakumbukwa Mtoto huyu mkubwa wa Jamal Khashoggi, Salah Bin Jamal Khashoggi mwenye uraia wa nchi mbili Saudi na Marekani (hati ya kusafiria) passport yake ya kusafiria ilizuiwa (restricted/banned) na Serikali ya Saudi mapema saada baada ya Baba yake alivyoanza kuandika na kukosoa  dhidi ya Kiongoz wa Saudi (prince) na serikali yake kupitia Gazeti la Washington post la  huko Marekani.


Ila siku za hivi karibuni, Sekretari wa ikulu ya marekani Mike Pompeo aliiomba Saudi arabia kuachia hati ya kusafiria ya mtoto huyo ,na hatimaye waliachia na sasa mtoto huyo tayari ameondoka kuelekea Marekani na taarifa zimetolewa kuwa tayari amefika marekani tangu Jana.


Suala la Mwili wa Khashoggi kupatikana katika Bustan ya Nyumba ya Balozi wa Saudi huko Istanbul ,Uturuki.


Taarifa hii Kwa mara ya kwanza ilitolewa na ,shirika la habari la Sky News kupitia Twitter ,siku ya jumanne,kuwa mwili umepatikana umekatwa katwa na sura kuharibiwa ngozi .


Na ndio kila shirika la habari likawa linasambaza habari hizo , kupitia chanzo cha SKY news(twitter).


Ikaja ikatia uzito mkubwa baada ya Rais wa Chama cha mlengo wa kushoto, (left-wing) VITAN PARTY  nchini uturuki,Mr.Dogu Perincek alipohojiwa na Kituo cha Television cha uturuki (Turkish Television) naye akathibitisha hivyo.


Ila Maafisa upelelezi na ofisi ya  mashtaka wa Uturuki hawakuweza kuthibitisha hilo na walikana kwa kusema "taarifa inayosambazwa kuwa mabaki ya viungo vya Muandishi Jamal ,vimepatikana sio kweli ,taarifa hizo ni fake .


" Instanbul Prosecutor's office denied that Khashoggi remains found at the Consul General's home ,picture of Social media is fake corps. hata Waziri Mkuu wa wingereza Theresa Mayi  alisema haya "The unconfirmed reports about the remains being found were “deeply disturbing " kuwa taarifa ambayo haijadhibitishwa kuhusu mabaki ya viungo vya Khashoggi inatia wasiwasi sana" 


Ila walitoa taarifa kuwa wamebahatika kupata Suitcase mbili (mikoba miwili) yenye vitu vya Khashoggi wakati wanafanya search katika Gari la ubalozi wa Saudi huko Instanbul ,Uturuki.


"Crime scene investigation found two suitcase personal belongs of Khashoggi during search of saud Consulate vehicle in Instanbul"


Upande wa mataifa makubwa ya ulaya na Marekani, wao pia wanasubiri uchunguzi kamili ukamilike ili waangalie ni adhabu ipi Saudi inapaswa ipewe na pia vikwazo vipi (sanctions) iwekewe ila mapema wiki hii ,Serikali ya marekani ilisitisha Visa kwa maafisa 21 wanaokisiwa kuhusika na kifo cha Khashoggi.


"US to revoke visas and consider sanctions against those responsible for Khashoggi killing"


"Those actions include revoking visas and entering visa lookouts, Mike Pompeo said, as well as working with the Treasury Department to consider slapping Magnitsky sanctions on those involved in the dissident journalist's slaying" alisema sekretari wa ikulu ya Marekani Mike Pompeo. Pia akimalizia kusema wakiendelea kusubiri taarifa kamili ,pia kazi inabakia kwa CONGRESS kuangalia adhabu zipi zinafaa kwa Saudi Arabia .


Ila kumekuwa na ukinzani kati ya matakwa ya Congress na matakwa ya Rais Trump juu ya Vikwazo kwa Saudi pale taarifa yote itakapotolewa Rasmi,tutajua zaidi .


Huko Uingereza pia Waziri Mkuu ,Theresa Mayi naye amezuia Visa kwa watuhumiwa wote wa mauwaji ya Khashoggi na kusema na wale ambao hawakuwa nayo hiyo visa hawatakiwi kuipata miongoni mwa watuhumiwa wa mauwaji,hawaruhusiwi kuingia Uingereza.


"The home secretary is taking action against all suspects to prevent them entering the UK and if these individuals currently having visas, those visas will be revoked today." said  Theresa Mayi.


Uchunguzi unaendelea taarifa kamili kusubiriwa itolewe juu ya kifo cha Khashoggi.


Pia Mchumba wa Khashoggi, Bibi Hatice Cengiz akihojiwa katika kituo cha Television  Haber Turk ,amekiri kukataa mualiko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutembelea Ikulu ya

 marekani,kupitia kwa sekretari wa ikulu ya Marekani Mike Pompeo .


Amedai kuwa "Rais,Trump amenialika kwenda ikulu ya marekani ila mimi nachukulia kuwa Tamko hili ni la kutaka kuonesha huruma kwa umma"


"Trump invites me to united states but l perceived it is a statement to win public favour"  Idont think of going to the united state ,whether I will go or Not wil depend on the formation of conscience "

Yeye anadai Trump hana nia thabiti kusaidia katika Jambo hili dhidi ya Saudi Arabia.


mwishoni mwa wiki iliyopita Mchumba huyo alikaririwa akisema kama Trump ataonesha jitihada za kufichua na kuchukua hatua juu ya yaliyotokea katika ubalozi wa Saudi nchini Uturuki, Instanbul juu ya kifo cha mchumba wake basi ataridhia mualiko huo.


if Trump "makes a genuine contribution to the efforts to reveal what happened inside the Saudi consulate in Istanbul that day, I will consider accepting his invitation."

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post