UVCCM Dodoma Mjini watembelea hospital ya Mirembe

 

Na Doreen Aloyce, Dodoma


KATIKA kuadhimisa miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM ,Umoja wa Vijana wa Chama hicho UVCCM Wilaya ya Dodoma wametembelea Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kwa ajili ya  kuwajulia hali wagonjwa,kupanda miti pamoja na kufanya usafi.


Akizungumza kwenye zoezi hilo jana  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Dodoma Said Kasote amesema kuwa Katika kuazimisha miaka 45, ya kuzaliwa Chama hicho ,wameona kutumia fursa hiyo kufanya kazi za kijamii ambazo zitaweka alama kwa Taifa.


Kasote amesema kuwa waliamua kwenda kwenye hospital hiyo ya Mirembe kwani ni  eneo la kimkakati ambalo limesahaulika na Jamii ambapo inaonekan kama hosptiali ya Wilaya jambo ambalo sio sahihi .


"Chama chetu Cha Mapinduzi  CCM ni Cha kijamii tunaamini Katika ujamaa na kujitegemea  hivyo tumefanya tukio hiki kwa ajili ya  Kutoa motisha kwa jamii hususani  kupanda miti ,kufanya usafi kutembelea wagonjwa jambo ambalo linatia Moyo na ishara ya Upendo Katika maisha yetu" amesema Kasote.


 

Pia amesema Katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Chama hicho , Umoja wa Vijana Wilaya ya Dodoma wako mstari wa mbele na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ,Rais Samia Suluhu Hassan kumpigania ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi .


Jaskon Mjinja ni Katibu wa Afya Hospital hiyo ya Mirembe amesema Umoja huo wa Vijana wamefanya kitendo Cha kihistoria kutoa huduma Kwa wagonjwa kwani hivi Sasa wamesahaulika kwa jamii ukizingatia afya ya akili ni jambo kubwa sana Kitaifa.


Amesema Jamii imekuwa ikichukulia vibaya hospital hiyo kuwa imejikita Kwa wagonjwa wenye afya ya akili jambo ambalo sio kweli Bali huduma zote zinatolewa na Kuna wataalamu Wengi nakuwataka wananchi wenye uhitaji wa kushauriwa kisaikolijia kufika kwa ajili ya matibabu .


"Licha ya hayo tuna changamoto hususani za mazingira ,lakini tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya fedha za UViKO 19 ambapo tumejenga  ujenzi wa  emergency department na  ,ICU ambavyo yatakamilika mwezi wa pili mwaka huu"amesema Mjinja.


Akitoa maelezo juu ya huduma wanazozitoa Kwa wagonjwa wa afya ya akili Katika Hospitali hiyo , Mtaalamu wa Tiba Kazi kiongozi, Julia Dagwa amesema kuwa wanawafundisha kazi ndogo ndogo za kujiudumia ikiwemo kupiga mswaki,kuoga ,na kufua sambamba na shughuli za burudani.


"Lakini pia tuna shughuli za uzalishaji ambapo tunalima matunda ,mboga za majani lengo ni kuutafsiri ubongo kumtambua mmoja mmoja na kumrekebisha na baada ya hapo tunaangalia kama Kuna uwezekano wa kumruhusu kwenda nyumbani na kupitia elimu hiyo inawasaidia kuishi vizuri na Jamii inayowazunguka"amesema Julia


Kwa upande wao Vijana wa Umoja huo wamesema kupitia tukio Hilo wamejifunza mambo mbalimbali ya uzalendo na kushirikiana na shughuli za kijamii. Hata hivyo kilele Cha sherehe hizo za kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM  zinatarajiwa kufanyika Rasmi tarehe 5 February mwaka huu Mkoani Mara .This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post