Jamii yaaswa kuendelea kufuata masharti ya Uviko-19

 Na Doreen Aloyce, Dodoma


Jamii imetakiwa kuendelea kujikinga na magonjwa ya UVIKO 19 kwa kuchukua Tahadharu sambamba na kutambua tofauti iliyopo Kati ya Ugonjwa wa Mapafu TB na UViKO .


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Steps Tanzania ,Dkt Cyprian Magere wakati alipokuwa kwenye mafunzo kwa Asasi zisizo za Kiserikali ambazo zinatekeleza Afua za kifua kikuu, Ukimwi,na Kuzuia maambukizi ya UVIKO 19 Mikoa ya Dodoma na Simiyu.


Amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga lenga kuwajengea uwezo viongozi na wafanyakazi wa Asasi hizo ili waweze kuibua wagonjwa wa kifua kikuu na wale walioacha kuendelea na matibabu kwa kipindi hiki Cha Mlipuko wa UViKO 19.


"Katika mafunzo haya tunamalengo mahususi kwa viongozi kupata uelewa wa kutosha wa kufanya kazi zao za Kutoa huduma ya Kuzuia maambukizi ya kifua kikuu , Ukimwi Kwa kipindi hiki Cha korona na kupata stadi za kutosha hivyo kupitia mafunzo hayo ongezeko ya idadi ya watu kupata chanjo itakuwepo"amesema Magere.


Nae Ally Chionda Meneja wa program kutoka Taasisi ya Steps Tanzania amesema mafunzo hayo yamewezeshwa na Shirika la Amref Chini ya ufadhiri wa mfuko wa Dunia kupitia Fedha za UVIKO 19 kuwa kupitia mafunzo hayo yatasaidia watendaji kuwa na uelewa zaidi tofauti iliyopo Kati ya Ugonjwa wa UViKO 19 pamoja na kifua kikuu TB.


Ally amesema kuwa hapo awali waligundua changamoto kwa watoa huduma ngazi ya Jamii namna ya kuifikia Jamii kutokana na wasiwasi hivyo kuwepo mafunzo hayo utawafanya warudi kwenye mstari na kuendelea kuhamasisha watu kupata chanjo na kuendelea Kutoa huduma bila kupata maambukizi.


"Kulikuwa na uhitaji wa hii elimu kujua mahusiano ya Ugonjwa huo, tunatambua mtu mwenye Kifua kikuu mtu akikohoa na yale maji maji yakimfikia mtu Ambaye Hana kifua kikuu Kuna uwezekano  wa kupata ugonjwa huo na pia mtu mwenye UVIKO 19 akikohoa na maji kumfikia Ambaye Hana yanaweza kumfikia haraka hivyo vyote vinashabihiana na hata dalili zinafanana"amesema Ally.



Akitoa elimu kwenye mafunzo hayo Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma Dkt Francis Bujiku amesema Jamii inapaswa kutambua kuwa  virusi waliowengi hawana Tiba ila Wana Kinga huku akibainisha  asili ya Virusi vya Corona 19 vimetokana na wanyama wakiwemo Paka,. Ngamia na Popo na kuenezwa kwa binadamu.


"Naomba niwaeleze kwamba ugonjwa wa Corona 19 hauenezwi kwa njia ya hewa bali inaenezwa kwa njia ya tone isipokuwa hewa inatusaidia kusambaza matone hivyo tuendelee kujikinga ili tusiambukizwe" amesema Dkt Bujiku .




Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamesema wataenda kuibua changamoto zinazosababisha watu wasichanje huku watumia fursa hiyo kuwapa elimu wananchi kutambua tofauti iliyopo Kati ya Ugonjwa wa Mapafu TB pamoja na UViKO 19 jambo ambalo litasaidia kupunguza vifo ninavyoweza kujitokeza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post