Watakiwa kupanda mazao yanayostahimili ukame

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Wakulima Mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia kanuni za kilimo Bora  ikiwa ni pamoja na kupanda mbegu za mazao yanayostahimili hali ya ukame ili kuwa na uhakika juu ya usalama wa chakula.


Kauli hiyo imetolewa na Afisa kilimo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Ansila Kalani ambaye amesema kutokana na utabiri wa Mamlaka ya hali ya hewa, hakutakuwa na Mvua za kutosha hivyo wakulima wanapaswa kuzingatia ushauri wa wataalam ili kulima kilimo chenye tija.


Ameeleza kuwa kwa mwaka huu 2021  Mvua zitakuwa chache,zitakazonyesha chini ya wastani wa kawaida hivyo wakulima wanapaswa kuchagua mbegu za muda mfupi yatakayoendana na hali ya hewa.


“Pamoja na mazao hayo wasisahau yale mazao yanayostahimili ukame mazao hayo ni Mtama, Uwele, Viazi vitabu, Mikunde pamoja na mazao ya bustani kwa maana ya kwamba yanamda mfupi lakini pia yanampa mtu kipato kwa haraka tunawashauri wakulima wazingatie ushauri wa wataalam  lakini pia wawatumie wataalam wa kilimo na mifugo walioko kwenye maeneo yao maana wataalam wameajiliwa kwa ajili ya kuwahudumia wao kwahiyo ni haki ya wakulima kama watahitaji elimu ya zao fulani wafike kwenye ofisi za kata waweze kuonana na wataalam watawasaidia”.


Afisa kilimo huyo ametumia nafasi hiyo kuwashauri wakulima kutunza na kuweka akiba ya chakula na kuepuka matumizi yasiyo sahihi kwa chakula.


“Ukiangalia msimu ambao tumepewa tahadhari kama hizi huko mbeleni hatujui inaweza kuwa hali ni mbaya zaidi kwahiyo niwaase  wananchi  wa mkoa wa Shinyanga watunze chakula walichonacho yaani waepuke yale matumizi ambayo siyo ya lazima kama kuna mtu anamchanganyiko wa Mahindi, Mpunga, Viazi, Mihogo na vyakula vingine anatakiwa ajue anatunza kiasi gani ili kiweze kumtosha kulingana na familia yake”.


“Nimuhimu kujua ni kiasi gani kinamtosha mtu mmoja kwenye familia kwahiyo mtu akichukua kile kiasi kama anaidadi ya watu kumi atajua atunze chakula kiasi gani kwa mfano kama mtu atatumia tu Mahindi kula kwa mwaka mzima mtu huyo atahitaji Mahindi gunia tatu za Mahindi na kama mtu huyo atakula wali tu mwaka mzima atakuwa anahitaji gunia tano za mpunga”.


Aidha Afisa kilimo huyo Bi Ansila Kalani amewaomba wakulima kuendelea kutumia samadi kwenye mashamba huku akiwasisitiza kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya mifugo yao.


“Huku jamii wengi ni wafugaji watumie samadi kwenye mashamba yao maana samadi inatusaidia kutunza unyevunyevu lakini pia wavune maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya mifugo  maana mifugo nayo itahitaji maji kingine wapande malisho na kuyavuna”.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post