Diwani kata ya Ndembezi atembelee miradi ya maendeleo

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Diwani wa kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga Victor Thobias amefanya ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo machinjio ya kisasa. 


Katika ziara hiyo diwani Victor amefuatana na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi pamoja na wataalam kutoka ofisi ya mtendaji wa kata ya hiyo ambapo kwa pamoja wametembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Mazinge, daraja la Mwanoni, ,mradi wa kufyatua matofali na Machinjio ya kisasa.


Diwani huyo amesema hatua za utekelezaji wa miradi yote waliyotembelea leo inaridhisha na kwamba inakwenda sanjali na kasi ya serikali inayotaka utekelezaji wa miradi yenye viwango vyenye ubora. 


”Kiukweli mambo naona ni mazuri kwa sababu barabara zinapitika kwa uzuri madaraja yanajengwa kwa kiwango kinachotakiwa na katika ziara yangu lengo  ni kutaka kuona je simenti inayotumika ni sahihi au wanalipualipua tu ili mwisho wa siku pasiwe na uimara wa kutosha lakini nimefurahishwa miundombinu ikovizuri”.


Amewaomba vijana kujitokeza ili kupata nafasi za kazi katika machinjio hiyo ya kisasa na kwamba Halmashauri itahakikisha inatoa fursa ya ajira kwa wananchi wote  na kwamba  kipaumbele zaidi ni kwa wazawa .

“Niwaombe wananchi hasa vijana wajitokeza kwa wingi kwenda kuomba kazi pale kwa maana ya kwamba ni vyema tukaanza na sisi hapa vijana wetu wapate ajira siyo hata kufagia tuletewe wafanyakazi wa mkoa mwingine wakati hizo kazi zinafaa hata kwa vijana wetu”.

Kwa upande wake katibu wa itikadi, siasa na uenezi kata ya Ndembezi Juliana Buzuruga amesema ujenzi wa miundombinu yote iliyotembelewa na kukaguliwa leo inaridhisha kutokana kutekelezwa kwa kiwango stahiki.


“Kwa kweli tumefurahishwa barabara zimetengenezwa vizuri pia tumekwenda mpaka kwenye ambalo linaunganisha kivuko palikuwa korofi zaidi ya miaka kumi iliyopita tumetoka pale darajani tumekwenda mpaka machinjio ya kisasa ambayo yapo mtaa wa Ndembezi kata ya Ndembezi tumefika pale tumezunguka kila sekta kwa kweli machinjio ya pale imekamilika”.


Mhandisi wa majengo wa kampuni ya Home Afrika Investiment Corporation Ltd Kassim Ibrahim ametoa wito kwa wananchi kuutunza mradi huo wa machinjio ya kisasa pindi utakapoanza uzalishaji na kuepuka kufanya hujuma za aina yoyote. 


“Hii ni machinjio ya wanashinyanga pindi wanapokuwa  kwenye maeneo kama haya ni ile tu kwamba kuwa waaminifu pale ambapo wanapoaminiwa kuja kufanyakazi huku”.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post