MKURUGENZI CRDB AELEZEA MIKOPO CHECHEFU ILIVYO PUNGUA, AIPONGEZA SERIKALI


Na Lucas Myovela, Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Abdulmajd Mussa Nsekela, amesema benki hiyo imepunguza mikopo chechefu ambayo imekuwa ikiumiza wateja wake na kushindwa kufanya marejesho.

Nsekela ameyasema hayo Leo Jijini hapa


wakati akitangaza kufanyika kwa Mkutano wa 26 wa wanahisa wa banki ya CRDB unaotakiwa kuanza kesho kutwa Jijini hapa na kujadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

"Katika mkutano Mkuu wa mwaka jana tulikubalina mambo mbalimbali ya utekelezaji kwa ajili ya ukuaji wa Banki yetu  ikiwemo kuchagua viongozi wa kuongoza mikutano ya wanahisa kwa ngazi ya Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti". Ameeleza Nsekela.

"Katika Mkutano Mkuu utaofanyika May 22,2021 utatanguliwa na semina ya kuwajengea uwezo wanahisa utakao fanyika May 21,2021 katika ukumbi wa AICC ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba". Amesema Nsekela

Pia Nsekela amesema licha ya Taifa letu kukumbwa na janga la ungonjwa wa Covid 19 imeweza kuongeza ufanisi zaidi katika utendaji na kupata mapato ya Bilioni 165 baada ya kodi kwa mwaka 2020.

"Mbali na changamoto ya ugonjwa wa Covid 19 tuliweza kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo mazuri lakini shukrani kubwa ni kwa Serikali kwa kupitia wizara ya fedha kwa kuweka mikakati bora kwa maendeleo ya mabeki hapa Nchini". Aliongeza Nsekela.

"katika swala la mikopo chechefu ambayo urejeshaji wake inasumbua imepungua kwa kufikia asilimia 4.4 kulinganisha na mwaka 2019 ilikuwa asilimia 5 kulinganisha na mwaka 2018 ambapo ilikuwa asilimia 9". Amesema Nsekela.

Pia Bw Nsekela ameeleza kuwa uchumi wa benki hiyo ya CRDB inaendelea vizuri kwa kota ya kwanza ya mwaka huu wamepokea faida ya shilingi Milioni 44.

Mkutano mkuu wa 26 wa CRDB wa wanahisa utakuwa na kaulimbiu isemayo PAMOJA HATUA KWA HATUA na Mkutano huo utafanyika May 22,2021 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post