SERIKALI KUPANUA WIGO WA INTERNET NCHINI KUANZIA 3G KWENDA JUU-WAZIRI DKT NDUNGULILE

 WAZIRI wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Mhe Dkt Faustine Ndungulile akijibu baadhi ya hoja za Wabunge Bungeni Jijini Dodoma

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira akisisitiza jambo  bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia

NA MWANDISHI WETU, DODOMA.

WAZIRI wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Mhe Dkt Faustine Ndungulile amesema Serikali itaongeza wigo wa Internet nchini na minara yote itakuwa inajengwa  kuanzia  3G kwenda juu ili kuwawezesha watanzania walio wengi waweze kupata huduma ya mtandao mpaka wananchi wa vijijini ili kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kujiletea maendeleo yao

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira ambaye aliishauri Serikali ipanue wigo wa Mtandao wa Internet ili wananchi wa mikoa ya pembezoni na vijijini nao waweze kunufaika na fursa zinazotokana na huduma hiyo.

Waziri Dkt Ndungulile alisema mwanzoni walipokuwa wanaanza mikakati yao ilikuwa ni kuhakikisha mawasiliano maana mitano yote ilikuwa ni 2G hivyo wamekubaliana kwa sasa minara yote inayokwenda kujengwa inakuwa 3G kwenda juu

Alisema kwani Dunia hivi sasa inaongelea masuala ya Digital Economy na ukiangalia miaka 10 iliyopita makampuni makubwa duniani yalikuwa kwenye manufacturing lakini sasa hivi ukiangalia yapo kwenye sekta ya Tehama hivyo kama nchi lazima waangalie huko.

“Kujibu swali hili la Mhe Neema Lugangira tupo kwenye maandalizi ya kuandika Digitali Economy Blue Print ya Tanzania na kazi hiyo imeshaanza hatua za awali na tunatarajia andiko litaanza hivi karibuni, sambamba na kuangazia e-commerce ”Alisema Mhe Dkt. Ndugulile

Waziri huyo hataki kukumbukwa kwamba alikuwa akiminya Sera ya Sekta hiyo badala yake akumbukwe kwa kufanya mazingira wezeshi ya Tehama kukua ndani ya nchi lakini niwaambie Wabunge kwamba tunakwenda kufanya mabadiliko makubwa sana ya kimuundo ya taasisi zake na muundo wa kisheria.

Alisema ikiwemo pamoja na vijana wanaojiajiri kupitia Tehama kwa vijana  akitolea mfano vijana ambao ni ni MC anafanya shughuli za harusi anarusha picha youtube ili watu waione umahiri wake wa kazi halafu anataka kutozwa kodi hilo wanataka kulikataa

Aidha alisema pia wasanii wanatoa kazi zao wanaziweka kwenye mitandao wao wanakwenda kuwaminya wanataka kwenda kufanya maboresha makubwa ambayo yataweka mazingira wezesehi kuhakikisha platfomu zao hawawezi kuzuia bali wawe wanakwenda ili vijana hao waweze kujiajiri.

Katika hoja yake pia Mbunge Neema Lugangira aliishauri Wizara kuona mana gani itaweza kupunguza ghamara zinazolipwa na Watanzania hususani hawa vijana kwa sababu hivi sasa ni changamoto kubwa.

Pia aliitaka Wizara ifanye mapitio ya sheria ili kuona namna gani ya kuondoka baadhi ya makosa kutoka makosa ya Jinai kuwa makosa ya madai maana yenyewe inaleta changamoto kubwa sana kuhakikisha watu wamenufaika na sekta hiyo.

“Lakini pia waongeze eneo la ufikaji wa internet kama wengine walivyochangia hususani vijijini hata wakifikie 3G kwa sababu interneti inasaidia kufanya biashara kwa vijana na wanawake na ukiingia mtandao wa Instragamu inasaidia sana lakini fursa hizo haziwasaidia wanaotoka maeneo ya pembezoni.

Mhe Neema Lugangira akisema pia lakini bado gharama za kupata internet hapa nchini ni kubwa ukilingananisha na nchi jirani mfano Nairobi gharama ya uzito kwa mwezi ni Dola za Kimarekani 5.5, Uganda kwa maana mji wa Kampala ni Dola za Kimarekani 10 na Tanzania kwa maana Dar es Salaam ni Dola za Kimarakeni 15.5 kwa hiyo unaweza kuona ulinganishi huu hivyo ni muhimu kufanya uangalizi wa gharama hizo.

Aliongeza kwa hali ilivyo watanzania wengi hawafaidi na hawanufaiki na sekta hiyo na Wizara ikiweza kufanyia kazi ushauri anautoa wataipunguzia mzigo Serikali wa ajira kwa vijana kwa sababu vijana watatumia Sekta hii kujitengeneza ajira.

“Natoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassam kutokana na mwongozo na nia yake kuhakikisha miundombinu ya teknolojia ya mawasiliano inafika asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 hayo ni maono makubwa ambayo yatapelekea kuimarisha uchumi wetu zaidi eneo la teknoloji ya mawasiliano” Alisema Mbunge Neema Lugangira

Alisema kwa sababu ni sekta muhimu ambayo ikiangaliwa kwa umakini nchi inaweza kupata kipato kikubwa pamoja na kutengeneza ajira  akitolea mfano Kenya sekta ya teknolojia ya mawasiliano inachangia asilimia 8 ya pato ghafi la Taifa na tayari sekta hiyo kwa Kenya imeshatengeneza ajira 250,000 na hiyo ni kwa mujibu wa Takwimu ya Serikali ya Kenya.

Mbunge Neema Lugangira alisema ukuaji wa sekta ya ICT Kenya umepitia ukuaji mkubwa kupita sekta zote kwa zaidi ya asilimia 23 na hiyo ni kwa mlongo uliopita pekee lakini kwetu Tanzania bado kuna changamoto ambazo wakiziangalia vizuri zitasaidia kuongeza ajira kupitia sekta hiyo ambazo hivi sasa imefungwa.

“Mfano mdogo wachangiaji wengi asubuhi walizingumzia suala la Youtube na YouTube hivi sasa kwa Tanzania mazingira yake sio rafiki nasema hivyo kwa sababu wapo wana mziki wachache au wadau ambao wanatumia YouTube akiwemo Diamond, Alikiba na Milladayo ambao wamenufaika lakini baada ya kuwepo kwa sheria ambazo zimepelekea changamoto watu wengi wamejiondoa kutumia mtandao huo ikiwemo vijana” Alisema

Mhe Neema Lugangira alisisitiza kuwa hiyo inaleta changamoto kubwa kwa sababu vijana wanatumia teknologia hiyo na sekta hiyo kujipatia ajira ambazo ni changamoto hivyo Sera zetu lazima ziweke Mazingira ya kuwawezesha wao kujiajiri.

Aliendelea kusema "Pamoja na changamoto hizo tofauti na nchi zingine hapa Tanzania vijana wetu wengi waliopo kwenye sekta hiyo hawana elimu rasmi ya masuala ya kidigitali hivyo tunavyowaongezea gharama za kulipa ni kufifisha jitihada zao binafasi ambazo wamezichukua kama vijana kujitengeneza ajira” Alisema

Mbunge Neema Lugangira alisema katika hili naomba niishukuru Kamati maana nao wamelisemea hilo na ushauri wangu wa tano naiomba Serikali iangalia namna ya kushirikiana na wabunifu ili kuongeza faida inayopatikana kupitia sekta hiyo waone namna gani ya kuweza kushirikiana nao na kuomba Wizara isijifungie na katika hilo naomba nimpongze Mh Spika, Mhe Job Ndugai kwa jithada zake kufungua milango ambapo alieleza awali Mhe Spika alikutana na vijana ambao ni wabunifu wakatengeneza app iliyokuwa inawezesha vijana na wananchi kuwa karibu na wabunge wao hivyo wizara ikishirikiana na hao wabunifu inaweza kuleta tija.

Hata hivyo alisema kwa kumalizia wanaweza kujifunza kwa wenzetu wa Kenya ambao wana Sera ya Digital Economy Blueprint ambapo hivi sasa Tanzania hatuna Sera yeyote na hivyo aliishauri Wizara iandae  Sera Madhubuti ya  Digital Economy Blueprint mengi yatashindikana maana hii sekta inahitaji iwe na miongozo thabiti lakini iwe na njia ambazo zitahakikisha inawalinda  watumiaji na walaji wa sekta hiyo alimuomba Mhe Waziri anapokuja kuhitimisha Hoja yake ya Bajeti ya Wizara yake aeleze ana mpango gani wa kuja na Sera ya Digital Economy Blueprint.
This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post