MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA KANDA WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)

 Na Mwandishi Wetu.


 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ikishirikiana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) imeendesha warsha kwa ajili ya viongozi wapya wa kila kanda (chapter leaders). Warsha ni ya siku mbili, tarehe 20-21 Mei 2021, jijini Dodoma katika ukumbi wa African Dream Hotel.Warsha hii inahusisha mafunzo juu ya kesi za haki za kibinadamu na kesi za kimkakati. Viongozi wa kikanda watapewa mafunzo kamili juu ya fursa na taratibu za kimahakama katika kutetea haki za kibinadamu kupitia kesi mkakati. Vilevile mafunzo haya yanalenga kuwafundisha na kuwajengea uwezo wa kuogoza kanda zao. Moja wapo wa watoa mafunzo ni Mh.Jaji mstaafu Robert Makaramba.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post