Meshack afungwa Jela Maisha kwa kumlawiti mtoto wa bosi wake, ni aliyekuwa akimpeleka shule kwa Baiskeli

 JELA MAISHA KWA KULAWITI MTOTO WA MIAKA MINNE:


Mahakama  ya  Hakimu  mkazi  MKoa  wa  Tabora  imemuhukumu kifungo  cha  maisha aliyekuwa  akifanyakazi  ya kubeba  abiria  kwa  njia  ya  Baiskeli  mjini  Tabora  baada  ya  kukutwa na hatia ya  kumlawiti mtoto mwenye  umri  wa  miaka minne  ambaye  alipewa  kazi  na  wazazi  wa  mtoto  huyo  ya  kumpeleka  shule  na  kumrejesha  nyumbani.


Kijana  huyo  mwenye  umri  wa  miaka  21 mkazi  wa  Tabora  mjini  imedaiwa  mahakamani  hapo  na  Wakili  upande  wa  Jamhuri,  TITO  MWAKALINGA  kwamba  mshtakiwa  aliyefahamika kwa  jina  la  MESHACK   JAMES  alitenda  kosa  hilo  kinyume  na  kifungu  cha  154  Ibara  ndogo  ya  kwanza  na  ya  pili Julai 2, mwaka  huu alipokuwa  akimrudusha nyumbani  mtoto  huyo


Katika  maelezo  hayo  yaliyowasilishwa  mahakamani  na  Wakili  huyo  katika  shauri  hilo  la  ukatili  dhidi  ya  mtoto  Namba  89/2020 likionesha madai  ya  kumlawiti mtoto  huyo na  kutolewa ushahidi na mashahidi  watano  akiwemo  daktari  ambao  Mahakama imejiridhisha  pasi na  shaka  kwamba  kijana  MESHACK  JAMES  alimfanyia  ukatili  huo wa  kumlawiti  mtoto  huyo  wa  kiume akiwa nyumbani  kwake na  kisha  kumtelekeza  mtoto  nje  ya  Geti. 


Hakimu mkazi  Mkoa  wa  Tabora, JOVIN  KATO  ametoa hukumu hiyo akisema iwe  fundisho  kwa  watu  wengine  wenye  tabia  chafu  ambayo kimsingi  haikubaliki  katika  jamii  na  kwamba  inawadhalilisha  watoto kwa ujumla.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post