MAADHIMISHO YA WIKI YA USAFI WA MAZINGIRA, DC MUFINDI AFUNGUKA HAYA

 

Na Mwandishi Wetu

Maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira yanafanyika tarehe 19 Novemba kila mwaka nchini Tanzania ambayo ni sehemu ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira na malengo ya milenia (Lengo namba 7C – Afya na Usafi wa mazingira).Ujumbe wa mwaka huu wa siku ya maadhimisho ulikuwa ni “ZINGATIA MAHITAJI YA JINSIA KWA USAFI WA MAZINGIRA ENDELEVU”, Ujumbe huu unatuhamasisha kuwa na ushiriki wa pamoja kwa jinsia zote ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira lakin pia sisi sote kuungana katika kupambana na changamoto za uchafuzi wa mazingira utokanao na kutotumia vyoo bora, utunzaji mbaya wa taka ngumu na utiririshaji wa maji machafu lakini pia ni kuifahamisha jamii kuwa suala la usafi wa mazingira ni jambo nyeti kwa afya, ustawi na maendeleo ya kila mtu kwa maendeleo endelevu. Maadhimisho ya wiki iya Usafi wa Mazingira kwa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa yamefanyika katika kijji cha Kitelewasi kilichopo Kata ya Mbalamaziwa na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wadau wa usafi wa mazingira mkoani Iringa. 


Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa ni Mh Mkuu wa Wilaya Ya Mufindi Ndg Jamhuri William ambaye alisisitiza na kutoa wito kwa wadau waliopo mkoani Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi katika kuendelea kushirikiana katika miradi ya Maji, Afya na usafi wa mazingira.Aidha Mh Mkuu wa wilaya Ndg Jmahuri William aliwaomba shirika la PDF na UNICEF kuendelea kushiriki katika kampeni ya kuweka wilaya ya Mufindi katika hali ya usafi.

Akitoa shukrani mwakilishi wa UNICEF Ndg Remigius Sungu alisema kuwa UNICEF na wadau wake inatambua changamoto zilizopo katika program za WASH na itaendelea kushirikiana na Halmashauri kutokana na ufanisi na ubora wa kazi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo bora kwa shule za Msingi na vituo vya kutolea huduma za Afya.Akifafanua miradi inayoendelea mwakilishi wa PDF – Mufindi Injinia Elias Erasmus na Johaness Rumito walisema kuwa wamepata ushirikiano mkubwa toka kwa uongozi wa halmashauri katika utekelezaji wa miradi inayoendelea ya ujenzi wa vyoo bora kwa shule tano za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi za Malangali, Mpeme, Mninga B, Sadani na Lugodalutali na vituo vya kutolea huduma za afya vya Kasanga na Dispensari ya Igombavanu.Maadhmisho yalihitimishwa kwa shirika la PDF kugawa masinki ya Plastic yajulikanayo kama SATO na kutoa elimu ya namna ya kutibu maji ya kunywa kwa kutumia vidonge vya AQUA TABS ambayo ni njia rahisi ya kuokoa muda na rasilimali kuni kwa kuchemsha maji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post