MABONDE YA MTO PESI KUENDELEZWA KWA KILIMO CHA UMWAGILAJI

 

Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw.Pololeti Mjema akizungumza na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na waandishi wa Habari hawapo katika picha, Ofisini kwake mapema leo, kushoto, ni Mkurugenzi wa Idara ya Matunzo na Mafunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni.Baadhi ya wakulima wakiwa katika mafunzo wakisikiliza mada inayohusu sheria ya Taifa ya Umwagiliaji.Bibi wa miaka sabini na sita (76) Kulusumu Kapinga, akipalilia shamba lake la mpunga, lililopo katika bonde la mtopesi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo katika kata ya Litisha Wilayani Songea.Mhandisi Hassan Mndeme akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu faida ambayo wakulima wataipata baada ya mafunzo hayo 

Bw. Joseph Miti Mkulima wa zao la Mpunga katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga, akiongea kuhusu faida zinazopatiana kutokana na kilimo hicho, ambapo alisema kilimo cha umwagiliaji kimekuwa ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hao kwani wengi wamepata ajira na kuongeza kipato.
Na Mwandishi Wetu, Songea

Imeelezwa kuwa mabonde matatu yaliyopo katika Kijiji cha Nakahuga, Peramiho wilayani Songea yafanyiwe upembuzi yakinifu ili yaweze kutumika katika kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni hazina ya serikali ya kupanua eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta zaidi ya laki sita zinazo mwagiliwa kwa sasa mpaka kufikia hekta milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka 2025.

Hayo yameelezwa  mapema leo Mkoani Ruvuma na Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mjema wakati alipokuwa akizungumza na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya umwagialiaji waliopo mkoani humo katika ziara ya kuelemisha wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji za Nakahunga wilayani Songea, Hanga Ngadinda wilayani Madaba, nakimbande na Msanjesi wilayani Nyasa.

Bw. Mjema alisema kuwa Serikali kupitia wizara  yakilimo, ilishatoa fedha kupitia halmashauri husika ili uendelezaji ufanyike na inajenga miundombinu hii kwa gharama kubwa sana hivyo mtoe elimu kwa wakulima ili wajue umuhimu na namna ya kuchangia katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji ili kuwe na utunzaji na uboreshaji thabiti wa miundombinuhiyo.” Alisisitiza.

Aliongeza kwa kuwakumbusha wataalamu kusisitiza swala zima la utunzaji wa mazingira kwani wananchi ndo wanufuaika zaidi wa matumizi ya vyanzo vyamaji huku akiwaasa wataalam hao kuelimisha kuhusu migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya maji na siyo kuangalia katika kutunisha mfuko peke yake ili wakulima nao waweze kunufaika.

“Naamni mnaorodha ya maeneo yanayofaa zaidi kwa kilimo cha umwagiliaji kuliko kilimo cha kutegemea mvua.” Alisisitiza.

Awali akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wakulima katika skimu ya Nakahuga iliyopo Peramiho, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya uendeshaji na matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni alisema mafunzo hayo yatawasiadia wakulima katika kuelewa kuhusu sheria ya Taifa ya umwagiliaji ya mwaka 2013 na namna ya kuchangia tozo za huduma za umwagiliaji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post