DC KIHONGOSI:WAZAZI WALEENI VYEMA WATOTO WAKIKE,ACHENI TABIA YA KUWAKEKETA NA KUWABAGUA.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenani Laban Kihongosi akipokea maandamano ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika Leo katika Hiki la Arusha katika shule ya Sekondari Suye.
Afisa Maendeleo ya jamii Jiji la Arusha Mwanamsiu Ndosi akitambukisha baadhi ya wageni katika meza kuu.
Wanafunzi wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe juu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike pamoja na kaulimbiu
Baadhi ya wanafunzi kutoka mojawapo ya shile katika jiji la Arusha katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa
Baadhi ya wanafunzi kutoka mojawapo ya shule katika jiji la Arusha katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa yenye kauli mbiu isemayo Mwezeshe mtoto wa kike kwa Taifa lenye Usawa
Baadhi ya wanafunzi kutoka Mwanama sekondari wakifuatilia kile kinachoendelea kwa makini katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Kimataifa. 
Baadhi ya wanafunzi kutoka mojawapo ya shule katika jiji la Arusha katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa yenye kauli mbiu isemayo Mwezeshe mtoto wa kike kwa Taifa lenye Usawa
Wanafunzi wakiwa katika maandamano ya Amani yaliyoanzia Impala hadi Suye sekondari katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Kimataifa  
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule z asekondari na zile za Msingi katika Jiji la Arusha wlaioshiriki katika maadhimisho hayo ya mtoto wa kike katika shule ya Sekondari  Suye.
Wanafunzi wakifuatilia burudani mbalimbali katika siku ya maadhimishio ya siku ya mtoto wa kike Kimataifa katika viwanja vya shule ya Sekondari Suye
wanafunzi wakiwa katika maandamano ya amani kuelekea shule ya sekondari Suye.
Wanafunzi wakifuatilia burudani mbalimbali katika siku ya maadhimishio ya siku ya mtoto wa kike Kimataifa katika viwanja vya shule ya Sekondari SuyeNa.Vero Ignatus,Arusha

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanawalea watoto wa kike ,sambamba na kuacha tabia ya kuwakeketa watoto wa kike, kwani hali hiyo watashindwa kukidhi mahitaji yao wanapokuwa mtu mzima.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Kenani Kihongosi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa na kuitaka jamii kuachana na Mila potofu kwani zinamnyong'onyesha mtoto wa kike, na kumsababishia kushindwa kukidhi mahitaji yake anapokuwa mtu mzima.

Aidha akitoa Wito kwa watoto wa kike kukuheshimu, na kusoma kwa bidii ili waweze kuja kuwa Viongozi bora wa baadae, katika Jamii yao

Kihongosi aliwakemea vijana na wazee wenye tabia mbaya ya kuwarubuni watoto wa kike, na kuwasababishia mimba za utotoni alisema yeyote yule atakayebainika, sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.

Nivoneiya Kikaho ni Afisa ustawi wa Jamii  Jiji la Arusha ,anasema kuwa  ukatili wa kijinsia umeongezeka sana katika Jiji la Arusha,ambapo alitaja sababu mojawapo inayochangia ni kutokuwajibika kwa wazazi,jambo amabalo limepelekea watoto kufanyiwa ukatili 

Pamoja na hayo alisema pia na watoto wenyewe wamekuwa tatizo  kutokuwa na nidhamu katika jamaa zao,na kutokutii kile wanachoambiwa na wazazi na walezi wao,jambo ambalo limewapelekea kuangukia mikono ambayo siyo salama .

"Watoto wetu hebu badilikeni ili mtimize ndoto zenu,msitamani maisha amabayo wazazi wenu hawajawalea kwayo,someni kwa bidiii,mtimize ndoto zenu,hayo maisha yapo ,someni kwa bidiii mtakuwa na maisha bora zaidi."alisema Kikaho 

Kwa upande wake Grace Muro mtaalam wa kuzuia ukatili wa kijinsi akutoka Shirika la World Education kupitia mradi wake wa Waache wasome, alisema kuwa mtoto anapotendewa ukatili anaathirika kisaikolojia,katika masomo yake hafanyi vyema,hata humpelekea kuingiwa na hofu hadi kuwaogiopa watu wengine, mwishowe anaweza hata kutoroka shuleni ili asiendelee na masomo yake

Muro alitoa wito kwa waaalimu kutokuwa wakali kupitiliza pale wanapoona mtoto amebadilika, badala yake wajenge ukaribu na kutambua chanzo cha tatizo,kwani wakati mwingine mtoto wa kike anapitia chamgamoto kutoka katika familia,ndugu wa karibu hivyo anakosa kufahamu mtu sahihi wa kumshirikisha ni nani kama ataona hata walimu wake wanakuwa wakali.

Akisoma risala iliyoandikwa nawatoto wakike kutoka shule zilizopo katika  Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa niaba ya wanafunzi wenzake Brenda Mallya ,alisema tatizo la ubakaji na ukeketaji bado umekithiri katika jamii, huku baadhi ya wakishirikiana  na mangariba , na kupewa Ardhi au kitu chochote chenye thamani ili kunyamazisha uovu huo na kumfanya mtoto wa kike kuwa amnyonge.

Risala hiyo iliendelea kusema baadhi ya ndugu huozesha watoto wakike wakiwa na umri mdogo,sambamba na kubaguliwa na kutokupewa haki ya kufanya maamuzi, kama wanavyofanya watoto wa kiume, pamoja na suala la mgawanyo wa Mali.

Aidha risala hiyo iliendelea kusema kuwa tatizo la mimba mashuleni,husababishwa na madereva bodaboda na baadhi ya ndugu wa karibu, kwasababu hiyo wanafunzi hao walitoa ombi lao kwa mkuu wa wilaya ya Arusha, kuunda tume kwaajili ya kushughukia changamoto zao ili waweze kutimiza ndoto zao za baadae.

Siku ya mtoto wa kike kimataifa huadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 ila kwa jiji la Arusha iliadhimishwa octoba 16/2020 katika shule ya msingi Suye ambapo maadhimisho hayo yalibeba kauli mbiu isemayo  Tumwezeshe mtoto wa kike kwa kujenga Taifa lenye usawa.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post