FCF wanasa watuhumiwa wa ujangili wa nyamapori za kitoweo

 

Na Mwandishi wetu, Arusha

 Opereseheni ya kuwasaka majangili wa nyamapori kwa ajili ya kutoweo imefanikiwa kukamata dWatuhumiwa 27 wakiwa na nyamapori,silaha za aina mbalimb,ali na vifaa vya kutega wanyamapori .


Operesheni ya kusaka majangili  katika pori la akiba Uvinza hilo zimekuwa zikifanywa kwa ushirikiano baina ya askari za kikosi cha kupambana na majangili(KDU) walinzi wa taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) na vyombo vingine vya dola.


Mkuu wa kitengo cha Ulinzi FCF, William Mallya  amesema watuhumiwa hao,wamekamatwa kati ya januari hadi Octoba katika maeneo ambayo FCF imewekeza uwindaji wa kitalii na uhifadhi.


Anasema kukamatwa watuhumiwa hao kumetokana na ushirikiano mzuri baina ya vyombo vyombo vya ulinzi lakini pia na wananchi.


"kutokana na elimu ambayo tumekuwa tukitowa juu ya masuala ya uhifadhi, wananchi wengi wamekuwa wakitoa taarifa zinazofanikisha kukamatwa kwa majangili"amesema


Mallya amesema watuhumiwa hao,baadhi wamekamatwa na nyamapori, mitego na silaha za Jadi na  tayari walifikishwa katika vyombo sheria na kesi zao zinaendelea kusikilizwa katika hatua mbali mbali.


Hata hivyo, ili kuzuia matukio ya ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo, Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA), imetangaza kuanzishwa utaratibu wa kuwa na bucha za nyamapori katika mikoa yote nchini.


Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA,Iman Nkuwi anasema tayari milango ya kuanzisha mabucha imefunguliwa nchi nzima na taratibu zimetolewa na akaonya majangili kuwa wataendelea kukamatwa


"Hakuna sababu ya kufanya ujangili kwani lazima utakamatwa ila sasa fursa imewekwa kufanya biashara halali ya nyama tunawaomba watu wajitokeze  kuomba na kufuata taratibu"amesema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post