CHADEMA YAPEWA ONYO KALI NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amekionya Chama kikuu Cha Upinzani ni CHADEMA kutokana na alichokiita Uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza Beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amekionya  Chama kikuu Cha Upinzani ni  CHADEMA kutokana na alichokiita Uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza Beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Msitaafu Jaji Mutungi ametoa onyo Hilo Mara baada ya Jana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wakati wakiendelea na vikao vya kupitisha jina la  atakaye peperusha bendera ya Chama Hicho katika nafasi ya Urais akisema hakutegemea kwa Chama kikongwe kikubwa Kama hicho kufanya kitendo hicho.

Amesema kwa mujibu wa katika ya Tanzania na Zanzibar ni kosa huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kumbuka kwamba Sheria hazijakwenda likizo.

Tangu siku ya Jumamosi Agosti mosi 2020 Vyama vya upinzani mbalimbali kwa Sasa vimekua vikiendelea na michakato ya kupitisha majina ya wagombea kwa nafasi mbalimbali

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post