AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH. MILIONI 5 BAADA YAKUKUTWA NA HATIA ZA KUMTUSI RAIS MAGUFULI MTANDAONI


Mkazi wa kijiji cha Nzoka, Wilayani Momba, Mkoani Songwe Fadhili Silwimba, amehukumiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 5 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtusi Rais Dkt John Magufuli katika mtandao wa facebook.

Kesi hiyo namba 117 ya mwaka 2019, imesomwa Mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, na kusema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 23 (1) na (2) cha mwenendo wa makosa ya kimtandao namba 4 ya mwaka 2015.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali Flavian Leonard Chacha, alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo, mnamo Septemba 7, 2019, kwa kutuma ujumbe wa kumtusi Rais kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post