WAZIRI LUKUVI AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUPIMA MAENEO YAO


WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi amezitaka Taasisi za Serikali kupima maeneo yao ili kuzuia uvamizi wa wananchi wanaowazunguka.Mwandishi Esta Macha anaripoti kutoka Mbeya 


Lukuvi ameyasema hayo katika Uwanja wa Maonesho wa John Mwakangale Jijini Mbeya wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nane Nane mwaka 2020 ukijumuisha mikoa ya Nyanda za Juu.

Hata hivyo Lukuvi ameagiza viwanja vyote vya maonesho nchini kupimwa na pia vilipe kodi ya Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Mstaafu, Nicodemus Mwangela kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa amepongeza uamuzi wa Waziri Lukuvi na kuahidi kusimamia.

Awali hati zilikuwa zikitolewa ofisi za Kanda ambapo kwa sasa hati zinatolewa katika ofisi za mikoa hivyo kupunguza urasimu wa upatikanaji wa hati kwani hivi sasa hupatikana katika kipindi kisichozidi siku saba.

Mwisho.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post