
Baada
ya kuteuliwa Bw. Mishustin alitoa hotuba kwenye baraza la chini la
bunge, na kuwashukuru rais Putin na baraza hilo kwa uungaji mkono wao,
pia amesema ataripoti sera za serikali mpya kwa baraza la chini mnamo
mwezi Aprili mwaka huu.
Vilevile amewaambia waandishi wa habari kuwa atakabidhi orodha ya mawaziri kwa rais Putin hivi karibuni.
Waziri mkuu wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Baraza la usalama la Urusi.