
Waziri wa kilimo na rasilimali ya wanyama wa Rwanda Bibi Geraldine Mukeshimana amesema, wizara yake iko tayari kukabiliana na uvamizi huo wa nzige.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema, nzige wameharibu karibu hekta 70,000 za mashamba nchini Somali na Ethiopia, na kutishia utoaji wa chakula katika nchi hizo.