
Jeshi
la polisi mkoani Kagera linamshikilia Juma Daniel, mkazi wa Kijiji cha
Kazingati kata ya Keza wilayani Ngara, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake
wa kumzaa, mwenye umri wa miaka miwili.
Daniel
anadaiwa kumuuwa mwanaye huyo kwa kumchoma moto usoni na makalioni na
kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali sehemu za haja kubwa, baada ya mtoto
huyo kujisaidia haja kubwa kitandani wakati wamelala.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema kuwa Baba huyo
alikwishatengana na mama mzazi wa mtoto huyo na kuoa mke mwingine.