TANZANIA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU)


Wa kwanza kulia ni Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)kulia kwake ni Dkt. Jim Yonazi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)
Wa kwanza kulia ni Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)kulia kwake ni Dkt. Jim Yonazi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)Eng. Clarence Ichwekeleza, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano).
Baadhi ya waandishi wa habari waluihudhuria semina iliyoandaliwa na PAPU kupata uelewa namna ya Posta inavyofanya kazi na shughuli mbalimbali za kimaendeleo
Baadhi ya waandishi wa habari waluihudhuria semina iliyoandaliwa na PAPU kupata uelewa namna ya Posta inavyofanya kazi na shughuli mbalimbali za kimaendeleo
Na.Vero Ignatus,Arusha
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 40 ya umoja wa Posta Afrika PAPU ambapo yatafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 17 -19 jan 2020 katika kituo cha Kimataifa cha mikutano AICC

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mwasiliano(sekta ya Mawasiliano),Dkt Maria Sasabo aliyasema hayo alipokuwa akizindua semina ya siku moja ya waandishi wa habari yenye lengo ya kuwajengea uelewa katika sekta hiyo  ambapo alisema  mkutano huo wa utahudhuriwa na  Mawaziri 45 kutoka nchi mwanachama wa PAPU ,Mashirika ya Kimataifa Mabalozi wa nchi na wananchama

Dk Maria aliesema kuwa Maadhimisho hayo ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika ni chachu nzuri kwao kufanya tathmini ya walipotoka ,walipo na wanapoelekea tangia kuanzishwa kwake mwaka 1980 .

Dkt.Sasabo ambaye alikuwa na Naibu Katibu Mkuu sekta ya Mawasiliano Dkt Jimmy Yonazi alisema siku ya tarehe 18 januari 2020 litawekwa jiwe la msingi la ujenzi wa jingo la ghorofa 16 la PAPU litakalogharimu shilingi biloni 33.5 ambapo ujenzi huo ni ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na PAPU.

Aidha alisema kuwa maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na uhamashishaji wa usajili wa laini za simu kwani zoezi hilo linatarajiwa kufikia tamati January 20 mwaka huu hivyo kila mwenye simu anapaswa kusajili kabla ya simu ambazo hazijasajiliwa kuzimwa.

Amewasihi wananchi kuzitumia vyema siku hizo 20 alizoziongeza Mhe.Ris Dkt Magufuli ambapo zimesalia siku chache kufikia tamati hivyo wazitumie kwaajili ya kukamilisha usajili ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza hapo baadae

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele alikabidhiwa kiwanja cha kujenga jengo la PAPU barabara ya Arusha –Moshi na kumtaka mkandarasi kampuni ya Beijing Construction Engeneer kujenga Jengo hilo kabla ya muda wa miezi 30 kama mkataba unavyosema na sio vinginevyo.

Alisema kuwa mkandarasi anatakiwa kumaliza ndani ya muda au kabla ya muda uliopangwa na katika eneo la ujenzi hakuna kuingia mtu yoyote bali ni wale tu wenye kibali cha Wizara ya mambo ya Nje kwani eneo hilo ni la Umoja wa Mataifa

Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele alikabidhiwa kiwanja cha kujenga jengo la PAPU barabara ya Arusha –Moshi na kumtaka mkandarasi kampuni ya Beijing Construction Engeneer kujenga Jengo hilo kabla ya muda wa miezi 30 kama mkataba unavyosema na sio vinginevyo.

Aidha alisema jengo hilo linajengwa baada ya Umoja huo unaoundwa na nchi zaidi ya 45 za Afrika  kukubaliana kwa pamoja kuwa makao makuu yake yajengwe Tanzania Jijini Arusha.

“Baada ya makubaliano hayo Rais wa kwanza wa Tanzania marehemu Julius Nyerere alitoa eneo hili mwaka 1980, lakini miaka imepita kwa sababu
mbalimbali, lakini Rais John Magufuli amehakikisha maono hayo lazima yatimie na sasa ujenzi unaanza tunamshukuru sana,”alisema.

Maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa posta Afrika{PAPU} yatakwenda sambamba na kongamano la Mawaziri wa Nchi 45 wa sekta ya Mawasiliano litakalofanyika Jijini Arusha leo lengo ni kujadili tulikotoka,tulipo na kupanga mpango kazi wa miaka ijayo katika sekta hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post