TCRA YATOA MAFUNZO UTEKELELEZAJI WA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI KWA WATENDAJI MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA SINGIDA

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi  akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa wa Singida leo ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kulia ni  Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
 Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida, Michael Moses,akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi, akizungumza.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida, Michael Moses, akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Afya (RMO), Dkt. Victorina Ludovick.
 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda, akitoa taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea. 
 Afisa Masoko wa TCRA, Abdulrahaman Millas Issa, akitoa mada kuhusu anwani za makazi na postikodi.
 Afisa Mwandamizi wa TCRA, Dorice  Mhimbira, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakielekea Mtaa wa Ipembe mjini Singida kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
 Afisa Masoko wa TCRA, Abdulrahaman Millas Issa, akiwaelekeza washiriki wa mafunzo hayo namna ya kuandika namba kwenye nyumba katika mtaa wa Ipembe. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakielekea eneo la Kilambida lililopo Kata ya Kindai mjini Singida, ambalo nyumba zake zimejengwa bila ya kufuata mipango miji  kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
MPANGO wa kuweka mabango ya anwani za makazi na postikodi usifanywe kisiasa bali ufuate taratibu na sheria zilizowekwa.
 
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kwa watendaji  mamlaka za serikali za mitaa Manispaa za Mkoa wa Singida leo ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 
 
” Suala ili naomba lisifanywe kisiasa lifuate sheria na taratibu zilizopo kwani katika maeneo mengine lilichelewa kufanyika kutokana na wanasiasa kutaka majina yao yawekwe kwenye vibao vya mitaa” alisema Nchimbi.
 
Alisema mpango huu wa kitaifa ni muhimu sana kwani unasaidia wakati wa matukio ya dharura kama moto na kuwafuata wagonjwa katika maeneo yao yanayojulikana tofauti na ilivyo hivi sasa.
 
Nchimbi alitaja faida nyingine kuwa utaweka vizuri mipango miji katika maeneo wanayoishi wananchi na utapunguza migogoro ya ardhi na utambuzi wa watu wanapoishi na kupata huduma 
za kijamii kwa urahisi.
 
 Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwaomba wataalamu wa mkoa wa Singida ambao wamepata mafunzo hayo kwenda kufanya kazi hiyo kwa bidii na weledi huku wakiweka maslahi ya Taifa mbele.
 
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Antonio Manyanda alisema TCRA imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika mradi huo kama ilivyoelekezwa katika sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 ambayo inalenga kuboresha maisha ya watanzania kwa kupambana na umaskini.
 
Alisema mpango huo ulianza katika jiji la Arusha ambapo baadhi ya kata ziliwekewa miundombinu ya anwani kama sehemu ya mfano (pilot) na baada ya hapo uliendelea katika jiji la Dodoma ambapo ushahidi wa miundombinu unaonekana.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post