MBWANA SAMATTA AVUNJA REKODIMshambuliaji kinara wa klabu bingwa ya Ubelgiji KRC Genk na nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta jana usiku ametimiza ndoto yake ya kuifunga timu kubwa duniani ambao ni mabingwa wa Ulaya, Liverpool.Goli hilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania.

Hata hivyo, matokeo ya mwisho ya mchezo huo wa Klabu Bingwa Ulaya yalikuwa mabaya kwa Genk kwa kulazwa kwa goli 2-1.
Samatta, aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona mpaka wavuni katika dakika ya 40 ya mchezo.
Mshambuliaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Ulaya tayari ameshapachika magoli mawili katika mechi nne. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post