MAMIA WAJITOKEZA UZINDUZI MSIMU WA KILIMO NJOMBE

Na Joctan Agustino, Njombe


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Luth Msafiri amezindua rasmi msimu mpya wa kilimo 2019/2020 katika Halmashauri ya Mji wa Njombe akiwataka wakulima kuhakikisha Wanapima udongo ili kuongeza mavuno zaidi.

Uzinduzi huo Umefanyika katika Kijiji na kata ya Uwemba ambapo uliambatana na maonyesho ya Pembejeo za kilimo kutoka kwa wadau wa sekta ya kilimo mjini humo.

Pamoja na mambo mengine Mh Luth Msafiri amewaonya mawakala wa Pembejeo za kilimo wenye tabia ya kuwauzia wakulima Pembejeo feki  na wale wanaopandisha bei kiholela.

Bi Luth Msafiri Alisema kuwa Hatowavumilia wafanyabiashara wote wa Pembejeo za kilimo wanaojihusisha na vitendo vya dhuluma kwa wakulima kwa kuwauzia Pembejeo Feki hususani Mbegu za Mazao Mbalimbali.

Maonyesho hayo yalibeba kauli mbiu inayohamasisha wakulima wote kuwa na utaratibu wa kupima udongo kabla kupanda mazao yao Shambani kwa lengo la kuongeza Uzalishaji.

Uzinduzi kama huo umefanyika katika Halmashauri zote za Wilaya ya Njombe.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post