RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA SHIRIKA LA NDEGE LA TANZANIA ATCL ZA KUTOKA DAR KWENDA MPANDA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka kuelekea mkoani Dodoma kwa kutumia usafiri wa shirika la ndege la ATCL mara baada ya kumaliza ziara yake Mpanda mkoani Katavi.
Ndege ya ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi huku ikimwagiwa maji (water salute)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono vikundi vya ngoma na kwaya vya Mpanda mkoani Katavi kabla ya kuzindua safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 12/10/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, viongozi wa mkoa wa Katavi, Wabunge, Mawaziri na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa safari za Shirika la ndege la Tanzania ATCL kutoka Dar kwenda Mpanda mkoani Katavi leo tarehe 12/10/2019.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post