Na Joctan Augustino, NJOMBE
Mamia ya wananchi
wameshiriki matembezi katika viunga vya
mji wa Njombe ambayo yameandaliwa na halmashauri ya mji wa Njombe kwa lengo la
kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Mbali na
kuhamasisha zoezi la uandikishaji lakini pia halmashauri hiyo imetumia matembezi
hayo kama kumbukizi ya kifo cha miaka 20 cha baba wa taifa Mwl Julias Kambarage
Nyerere.
Awali
akizungumza katibu tawala wilaya ya
Njombe Emmanuel George pamoja na msimamizi wa uchaguzi hamashauri ya mji wa
Njombe Venance Msungu wanasema wam
elazimika kutumia mbinu ya kufanya matembezi katika viunga vya mji wa Njombe pamoja mazoezi ya pamoja ili kutoa hamasa kwa umma kujitokeza kujiandikisha .
elazimika kutumia mbinu ya kufanya matembezi katika viunga vya mji wa Njombe pamoja mazoezi ya pamoja ili kutoa hamasa kwa umma kujitokeza kujiandikisha .
Fullshangwe imezungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe ambao wameshiriki katika
matembezi hayo akiwemo Wilton Mwaisela
na Yasinta Kisima wanaeleza jinsi walivyo hamasika kujiandikisha na kutoa rai
kwa wengine kushiriki.


