Na Egdia Vedasto, Arusha
Waziri wa kazi Ridhiwan Kikwete amepongeza uongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini wa kabla ya uhuru na baada ya uhuru wa TUCTA kwa mafanikio makubwa ya kupata kitega uchumi hicho muhimu.
Amesema hayo Jijini Arusha na kutoa rai kwa wafanyakazi wote wa TUCTA kuenzi jitihada hizo muhimu ili matunda yake yakawafae kizazi hiki na kijacho.
"Mmekuwa mfano bora wa kuigwa na chachu ya mafanikio katika nchi hii, endeleeni kushirikiana na serikali na kuonyesha mshikamano wenu ili kuhakikisha wote kwa pamoja tunafikia malengo ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi",
"Nimefarijika kusikia tayari jengo lina wafanyabiashara 115, endeleeni kuaminiana, kuwajibika, kuimarisha imani kwa serikali yenu. Nawaasa shirika linalosimamia mali hizi la WCD kumbukeni kuwa TUCTA inategemea kitega uchumi hiki, hivyo kitunzeni na kukikudmisha ili kiwe kielelezo cha mafanikio"
Sambamba na hayo amewakumbusha kuzingatia haki za wafanyakazi wao, kuwasikiliza, kusimamia maadili na nidhamu, kufanya suluhu na mapatano.
Amesema ahadi ya serikali ni kuendelea kuongeza mishahara na kuhakikisha mapato yao yanaongezeka na kupandisha pensheni kwa wastaafu ili kufikia 2050 maisha yawe bora kwa kila mfanyakazi.
"Tumefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 katika yale tuliyoyapanga kuwafanyia wafanyakazi, ikiwemo hili la kuhakikisha wanaishi maishi bora kitokana na kupandisha mishahara" amesema Kikwete.
Amewakumbusha wafanyakazi kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa upande wake rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA Tumaini Nyamuhokya amesema ujenzi wa jengo hili ulioanza 1975 na kufikia leo linakamilika ni kwa jitihada kubwa za wadau mbalilbali shirikisho la vyama na serikali kwa ujumla.
Amesema kwa utaratibu, TUCTA hawaruhusiwi kufanya biashara kwa lengo la kulinda taratibu, hivyo jengo hilo litakabidhiwa kwa WDC kuendesha shughuli za jengo hilo.
Kwenye shirikisho lao vyama vimefikia 16, na wanaendelea kukaribisha vyama vingine vitakavyokuwa vimekidhi vigezo na taratibu.
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ongezeko la mshahara la asilimia 35.1kwa wafanyakazi wote nchini.
"Jengo hili lina vyumba vya kulala vya watu maaum, vyumba vya kawaida, hoteli na vyumba vya kufanyia biashara" amesema Nyamuhokya.
Hata hivyo jumla ya vyama 16 vinavyounda TUCTA vimepokea zawadi ya vyeti akiwemo Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi waandishi wa habari JOWUTA Mussa Juma.
Sambamba na hayo wametambua mchango wa wadau mhimu waliounga mkono juhudi zao za maendeleo ya kukakamilisha jengo hilo akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim kwa ushirikiano na mchango wake mkubwa kuhakikisha wanafikia mafanikio makubwa ya shirikisho.


