SHULE YA MECSONS YAJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA TANGU KUANZISHWA KWAKE

 

Na Egdia Vedasto,  APC TV 

Shule ya awali na msingi ya Mecsons yenye mchepuo wa Kiswahili nakingereza imeelezwa kujivunia mafanikio makubwa kwa kuwanoa wanafunzi kitaaluma na kitabia tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006 na kuwa moja ya shule zinazofanya vizuri nchini.

Akizungumza katika mahafali ya 14 ya shule hiyo Mkurugenzi wa shule hiyo Mecky Shirima amesema sambamba na kutoa taaluma kwa watoto waliokuwa wakijihusisha na kutoa misaada kwa watoto yatima, wazee wasiojiweza na wafungwa.

"Kipekee nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu kila mmoja, leo tunajivunia kwa pamoja mafanikio haya ya kuwa na wanafunzi 706 ukilinganisha idadi ya watoto 2 tulioanza nao mwaka 2006, nawasihi wazazi na walezi tuendelee kushirikiana kwa pamoja tuhakikishe tunasonga mbele" amesema Shirima. 

Ameongeza kuwa shule  imefanikiwa kutoa ajira za kutosha kwa walimu, madereva na wafanya usafi wengi wakitokea katika jamii inayozunguka shule hiyo. 

Wakisoma risala ya walimu kwa niaba ya walimu wenzake,  mwalimu Mosses Luheba amesema  kuwa shule hiyo imefanikiwa kupanda kitaaluma kila mwaka na kuwa katika nafasi ya daraja "A" kwa miaka minne mfululizo. 

Sambamba na hayo ametaja changamoto kadhaa ikiwemo kuzorota kwa ulipaji wa ada, ukosefu wa sare za skauti za kufanyia mazoezi na mwamko mdogo wa wazazi katika kuwahimiza wanafunzi kufanya mazoezi ya nyumbani. 

Mwakilishi wa Wazazi akitoa neno lake kwa wahitimu amewataka watoto kuwa watii na kutojiingiza katika makundi mabaya ili waweze kutimiza malengo yao. 

Mimi ni mfano bora wa walionufaika na shule hii, watoto wangu wote wamesoma hapa, na waleendelea kufanya vizuri katika masomo yao ya elimu ya juu, nawasihi wazazi tuendelee kushirikiana na walimu hawa ili kwa pamoja tuwalee watoto wetu na kusaidiana kutambua mabadiliko yao ya tabia na maendeleo yao ya shule. Pia ukiitwa mzazi itika wito ukawasikilize walimu maana mtoto analelewa kwa ushirikiano" amesema mzazi. 

Katika namna hiyo hiyo Leonard Lyatuu meneja wa CRDB tawi la Morombo, Arusha amewapongeza wazazi, bodi na walimu kwa juhudi za kulea watoto hao hadi kufikia hatua ya kumaliza elimu yao ya msingi. 

"Juhudi na ushirikiano wenu hakika umeleta mafanikio ambayo leo kila mmoja anajivunia, nami nawakumbusha wazazi  kuwekeza ada kidogo kidogo ili muweze kulipa ada mapema, hatua hiyo itamuwekea mtoto mazingira rafiki ya kusoma" amesema Lyatuu. 

Sambamba na hayo amewatakia kila la kheri katika hatua nyingine wanayoiedea, na kuwataka kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao na kuwa baraka kwa wazazi wao. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post