KUKATIKATIKA KWA UMEME CHALINZE KUMEMPONZA MENEJA TANESCO

 





Na Scolastica Msewa, Chalinze

Baraza la madiwani Halmashauri ya Chalinze limekataa kupitisha taarifa za utekelzaji wa mradi ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Bagamoyo kinachojengwa Chalinze nakusimamiwa na Mdhibiti wa ubora wa elimu Chalinze  pamioja na taarifa  ya Shirika la umeme TANESCO  baada ya baraza kutoridhishwa taarifa za  utekelezaji wa miradi zilizowasilishwa  na taasisi hizo kwenye Baraza hilo la Madiwani.


Akizungumza mara baada ya baraza kukataa kupokea taarifa za taasisi hizo mbili katika Baraza la madiwaani ambapo limefanya kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha mjini Chalinze Mwenyekiti wa halmashauri ya chalinze Hassan Mwinyikondo amesema kutokana na umuhimu wa miradi hiyo kwa Wananchi wa Chalinze na Wilaya nzima ya Bagamoyo taarifa zilizoandaliwa zilikuwa zikitia shaka.


Alisema Baraza hilo halijaridhishwa na taarifa hiyo ya Mdhibiti wa ubora wa Elimu halmashauri ya Chalinze na taarifa ya  shirika la umeme Tanzania -Tanesco halmashauri ya chalinze baada ya  baraza kupata shaka juu ya taarifa zilizowasilishwa na taasisi hizo na kuwapa agizo la kuandaa vema taarifa zao na kuwasilisha taarifa kwenye Baraza lingine kwa kuandaa kikao Chao Cha Baraza lao la Madiwani ambalo Taasisi hizo zitagharamia.


Alisema kuhusu ujenzi wa Chuo Cha Veta wilayani humo baraza limepata shaka juu taarifa zisizojitosheleza zilizotolewa na Mkuu wa idara hiyo Davis Moje na haendani kati ya fedha zilizoletwa.na serikali kuu na hatua ujenzi ilipofikiwa.


Kwa Upande wa Tanesco Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Chalinze alisema Wananchi wamekuwa na maswali mengi kutokana na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara na wao Madiwani hawana maelezo sahihi kuwajibu Wananchi.


Ambapo pia baraza hilo pia limemtaka wakala wa usimamimizi wa misutu TFS halmashauri ya chalinze kutoa majibu ya kero mbalimblia zinalalamikiwa na wananchi dhidi yao katika Baraza hilo watakalo andaa kwakuwa Meneja wake hakuhudhuria kabisa bila taarifa.


Alisema Madiwani ndio wawakirishi wa Wananchi katika Halmashauri hiyo hivyo wanatakiwa kuwa na taarifa sahihi na zakutosha ili wakaweze kuwafafamulia Wananchi katika Kata zao kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo muhimu kwa Wananchi wa Chalinze.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Halima Okash aliungana na Baraza hilo na kutoa maagizo juu ya maamuzi yaliiyofikiwa na baraza la madiwani dhidi ya taasisi ambazo taarifa zake zilikuwa na mashaka  na baraza la madiwani la halmashauri ya chalinze na kuagiza hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na vyombo vya usalama vifuatilie miradi hiyo na kama kutabainika ubadhirifu wowote hatua zichukuliwe dhidi yao.


Buge Angetile Meneja TARURA Wilaya ya Bagamoyo amesema ukarabati na matengenezo ya Barabara yalisitishwa kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha nchi nzima lakini Sasa kwa kuwa zimepungua utekelezaji utaendelea ili Barabara za Halmashauri hiyo zipitike vizuri muda wote.


Mdhibiti ubora wa Halmashauri ya Chalinze Davis Moje alisema Chuo Cha Veta Chalinze kinatarajia kugharimu shilingi bilioni 1.5 kwa kujenga majengo 9 kwa awamu ya kwanza ambapo tayari milioni 323 zimekwishaletwa kwa awamu mbili.


Alisema majengo hayo yamefikia hatua ya msingi na fedha kiasi zimetumika kwa ujenzi hatua ya msingi, kulipia mafundi na kununua vifaa vya ujenzi huo ambao unasimamiwa na Dar es salaam Institute of technology -DIT kwa kutumia wazabuni binafsi ambao walishinda kwenye zabuni.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post