CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KUFUNGUA BENKI HIVI KARIBUNI

_Ernest Nyambo Mwenyekiti wa Bandarini saccos_

 Na Egidia Vedasto

Arusha 

Chama Kikuu Cha Ushirika Tanzania kinatarajia kufungua benki mwezi Mei mwaka huu kutokana na kukua na kuimarika kwa vyama vya ushirika nchini.

Akizungumza katika jukwaa la mafunzo  yaliyowakutanisha viongozi wakuu wa vyama vya ushirika  akiba na mikopo (SACCOS) kutoka mikoa mbalimbali Dkt. Cathbert Msuya amesema kuwa Chama hicho kimeirika kwa  mfumo wa sheria zilizoko kwa sasa.

Aidha ameeleza kuwa Chama hicho kwa sasa kina akiba ya shilingi bilioni 16 ambapo kimevuka malengo ya kumiliki bilioni 15 ambazo ndio kiwango walichopangiwa na Benki Kuu.

Dkt. Msuya Amefafanua kuwa Benki Kuu imekishauri Chama hicho kuongeza kiwango kutoka bilioni 16 hadi bilioni 20 kiwango kitakachosaidia kuendesha shughuli za kibenki bila wasiwasi.

"Mafunzo haya naamini yamewaimarisha viongozi katika uendeshaji wa shughuli zao na yawatasaidia kukuza na kuboresha sera za vyama vyao jambo litakalowavutia watu wengine kujiunga  na vyama hivyo" ameeleza Dkt. Msuya.  


Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika Dkt. Cathbert Msuya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini arusha


Pia Chama Kikuu Cha ushirika kimekuwa kikichangia katika shughuli za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji na kusaidia zinazoishi katika umaskini.

Akifunga jukwaa la mafunzo hayo Leo jijini Arusha Mrajisi wa vyama vya ushirika, akiba na mikopo divisheni ya udhibiti iliyopo chini ya Wizara ya kilimo Collins Nyakunga amesema, msingi wa jukwaa hilo ni kukutanisha viongozi wa vyama vya ushirika ili kujadili mwenendo na changamoto wanazokumbana nazo.

Nyakunga ameendelea kufafanua kwamba jukwaa hilo limejifunza mambo mbalimbali ikiwemo kubadilishana mawazo, uzingatiaji wa sheria na taratibu, pamoja na matumizi sahihi ya TEHAMA.

Ameendelea kuwasisitiza viongozi wote waliojumuika katika jukwaa hilo kuhakikisha vyama vyao vinaingia kwenye mfumo wa TEHAMA ili kurahisisha shughuli za uratibu wa vyama lakini pia kuepuka upotevu wa fedha hatua itakayopelekea ukuaji zaidi wa benki inavyotarajiwa kuzinduliwa mwezi Mei mwaka huu.

"Naona  Chama kinafanya vizuri kinapiga hatua na wanachama wanapata manufaa makubwa mfano mwanachama akihitaji mkopo anaupata haraka tofauti na taasisi zingine, hivyo nashauri kanuni, sheria  na taratibu zizingatiwe lakini pia kudhibiti matendo yasiyofaa ili kulinda ushirika wetu" amesisitiza Nyakunga.

Nyakunga amesema viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu, waaminifu ili kulinda wateja wao na kuwajengea imani ya Chama sambamba na hayo ameongeza kwamba  itolewe elimu ya afya ya akili kwa wanachama, wafundishwe madhara ya rushwa na wapewe mafunzo mbalimbali yatakayoboresha vyama vyao.

Ameendelea kueleza kwamba hati safi kwa vyama  zimeongezeka na vyama 400 kati ya vyama 800 havijawasilisha taarifa za usajili  suala ambalo linazorotesha ukuaji wa ushirika huo. 

Mmoja wa viongozi kutoka Bandarini SACCOS Mwenyekiti  Ernest Nyambo amesema jukwaa hilo limeleta mabadiliko makubwa na uelewa wa wanachama tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Tunashukuru kwa sasa mifumo ya usimamizi  imeimarishwa na tuna imani kubwa na viongozi wetu wa sasa tofauti na miaka ya nyuma, hivi sasa mambo yote yanaendeshwa kwa mfumo hivyo mianya ya upotevu wa fedha  ni ngumu" ameeleza Nyambo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post