ZIARA YA KATIBU WA SMAUJATA KANDA YA ZIWA BWANA HASHIM OMARY ATOA ELIMU YA UKATILI KWA WANAFUNZI, SHULE YA SEKONDARI NGOKOLO, SHULE YA MSINGI LITTLE TREASURES NA WANANCHI MANISPAA YA SHINYANGA

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Katibu wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Kanda ya ziwa Bwana Hashim Omary amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia.

Ameyasema hayo leo wakati akitoa elimu ya ukatili kwa  wanafunzi, wananchi wakiwemo walengwa  wa Tasaf wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ambapo leo ametembelea shule ya sekondari Ngokolo, shule ya msingi Little Treasures ikiwa  ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Bwana Hashim Omary Ramadhan pamoja na mambo mengine amewasisitiza wananchi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia,lakini pia  amewataka viongozi kuepuka rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi amewakumbusha wazazi na walezi kuwajibikia jukumu la kuwalinda watoto dhidi ya ukatili.

Kwa upande wake Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) amesema serikali ya mtaa huo imeendelea kuchukua hatua dhidi ya watu wanaobainika kufanya ukatili.

Naye katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya amesema kampeni hiyo itaendelea kutoa elimu ya ukatili katika maeneo mbalimbali huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuibua na kutokomeza ukatili unaoendelea kwenye jamii

Leo katibu wa SMAUJATA kanda ya ziwa Bwana Hashim Omary

leo ametembelea shule ya sekondari Ngokolo, shule ya msingi Little amefanya ziara ya siku moja ambapo ameungana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga kutoa elimu ya ukatili ambapo ametembelea shule ya sekondari Ngokolo, shule ya msingi Little Treasures pamoja na kwamba viongozi wametoa elimu ya ukatili wanafunzi, wananchi wakiwemo walengwa  wa Tasaf wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Ziara hiyo pia imekwenda sanjari na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo viongozi wa SMAUJATA wamewashukuru viongozi wa serikali Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano wanaoendelea kuupata katika kupambana na ukatili.

Viongozi hao wamemshukuru mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Aidha viongozi hao wa SMAUJATA wamesema wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchochea maendeleo ambapo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutambua juhudi za kampeni ya SMAUJATA katika kupambana na uhalifu kwenye jamii.

Pia viongozi hao wamesema wataendelea kutekeleza maono ya Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Shujaa Sospeter Bulugu katika kutokomeza ukatili Nchini.

SMAUJATA ni kampeni huru ya kupinga ukatili Nchini ambayo ilianzishwa na Shujaa Sospeter Bulugu kwa kushirikiana na Waziri Dorothy Gwajima ambapo kampeni hiyo inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

 

Katibu wa SMAUJATA Kanda ya ziwa Bwana Hashim Omary na Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakizungumza na katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga baada ya kusaini kitabu cha wageni leo Jumanne Disemba 5,2023.Viongozi wa SMAUJATA baada ya kuwasili katika shule ya msingi Little Treasures iliyopo Manispaa ya Shinyanga.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post