THE SUNRISE NURSERY AND DAY CARE CENTRE MAHAFALI YA 3, KILA MWAKA WATOTO 5 KUSOMA BURE, MWENYEKITI HABIBA JUMANNE AHIMIZA WAZAZI NA WALEZI, SMAUJATA SHINYANGA YATOA ELIMU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wazazi na walezi wanaoishi na watoto chini ya umri wa kuanza darasa la kwanza katika Manispaa ya Shinyanga wameshauriwa kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya elimu ya malezi ya awali kwa watoto (Day Care) ili waweze kuwa na msingi bora wa elimu.

Ushauri huo umetolewa na Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu kwenye kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre, Mwenyekiti wa mtaa wa Kitangili Bi. Habiba Jumanne ambapo amesema ni muhimu watoto kupata elimu ya malezi ya awali kabla ya kuanza darasa la kwanza.

Mwenyekiti huyo Bi. Habiba Jumanne ametumia nafasi hiyo kuwaomba wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ya malezi ya awali ili kuwatengenezea misingi bora ya elimu wawapo shule ya msingi.

Akizungumza mkurugenzi wa  kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre kilichopo mtaa na kata ya kitangili Manispaa ya Shinyanga Bwana Ndaki Mathias amesema kila Mwaka kuna utaratibu wa watoto watano kupata elimu ya malezi ya awali bure  hasa wanaoishi katika familia zenye kipato cha chini.

Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo wamewapongeza na kuwashukuru walimu wa kituo hicho kwa kuwaimarisha watoto wao huku wakisema ni muhimu watoto kupata elimu ya malezi ya awali kabla ya kuanza darasa la kwanza.

Jumla ya watoto 27 wamehitimu Mwaka huu 2023 katika kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre kilichopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka awapongeza wazazi kwa kuwapa kipaumbele watoto katika suala la elimu huku akiwaomba wazazi na walezi kuwapelekea watoto shuleni ili kupata haki yao ya elimu.

Aidha Mhe. Nyangaka ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa kata ya Kitangili kuendelea kuchukua tahadhari ya Mvua nyingi zinazotajwa kuwa ni Mvua za El nino ambapo Mkoa wa Shinyanga ni moja ya Mikoa inayotajwa kuathirika na Mvua hizo.

Katika mahafali hayo viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga akiwemo Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya pamoja na Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa (Cheupe) wametoa elimu ya ukatili kwa watoto, wazazi, walezi na wananchi wote waliohudhuria sherehe hiyo.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wamewakumbusha wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mazuri huku wakiwasisitiza kuimarisha ulizi na usalama kwa watoto wawapo nyumbani lakini pia nje ya familia yao na kwamba hali hiyo itachangia kuwaepusha na ukatili.

Viongozi hao wameitaka jamii kuacha vitendo vya ukatili huku wakiwasihi kutoa taarifa za ukatili sehemu huzika au kupiga namba ya bure 116 kutoa taarifa za ukatili ili hatua za kisheria ziweze kuchukua kwa wahalifu.

Wametumia nafasi hiyo kuviekeleza vituo vya kulea watoto kuweka mabango yenye ujumbe wa kupinga ukatili katika mazingira ya shuleni au vituoni ili watoto waweze kuwa na tahadhari katika kuepukana na ukatili.

Viongozi wa kampeni ya kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wameendelea kutoa elimu ya ukatili sehemu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili.

 

Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu kwenye kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre, Mwenyekiti wa mtaa wa Kitangili Bi. Habiba Jumanne akiwasili ukumbini.


Wazazi, walezi na wananchi mbalimbali waliohudhuria mahafali ya tatu Mwaka huu 2023. katika kituo cha malezi ya watoto The Sunrise Nursery and Day Care Centre kilichopo Manispaa ya Shinyanga. 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post