SHIRIKA LA COMPASS LAPANDA NA KUGAWA MICHE YA MITI ZAIDI YA 400 KATA YA TINDE MKOANI SHINYANGA

Katika taarifa yake mkurugenzi wa shirika la Compass Rosemary Ndegeya amesema shirika hilo limegawa miche hiyo katika shule ya sekondari ya wasichana Tinde, shule  ya Sekondari Kituli, kituo cha afya Tinde, na Mamlaka ya Mizani kituo cha Tinde.

Mkurugenzi huyo amezihimiza taasisi hizo kuitunza miti hiyo ili iweze kukua na kuleta matokeo chanya katiki jamii huku akiiomba ofisi ya mazingira  kusimamia uendelevu wa utunzaji wa mazingira ili kufikia malengo.

“Compass Tanzania ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililoanzishwa mwaka 2022 chini ya sheria ya NGO Namba 24 ya mwaka 2002. Kama Jinsi tunavyojua kazi ya kifaa Compass yaani Dira, shirika letu lina ndoto ya kuwa dira ya mafanikio kwa wananchi wote Tanzania tukianza na Mkoa wa Shinyanga. Kauli Mbiu yetu ni… COMPASS TANZANI…. Njia ya mafanikio (the path to success)”.

“Dira yetu ni kuona  jamii iliyojengewa uwezo na yenye miradi ya kimaendeleo yenye matokeo makubwa ili kuifika ndoto yetu, Compass Tanzania imejikita katika shughuli za utunzaji wa mazingira, utetezi wa haki za binadamu na utekelezaji wa miradi yenye matokeo makubwa huku tukipinga aina zote za unyanyasaji wa kijinsia”. amesema Mkurugenzi Rosemary

“Malengo ya shirika hili ni kuhamasisha miradi ya ki maendeleo yenye ushiriki wa wanaichi na ufanya utetezi na ulinzi wa haki za binadamu hasa wanawake na Watoto Compass Tanzania inatekeleza shughuli zake Tanzania bara, kwa namna ya Pekee Tumeanza na Mkoa wa shinyanga, Taaasisi yetu ilitambulishwa Ngazi ya Mkoa na kupokelewa mapema mwaka huu 2023. Mara tu baada ya kupokelewa na kupewa kibali cha kutekeleza shughuli zake, Taasisi yetu kupitia meneja Miradi Mkoa wa Shinyanga ngudu Boniface Mhana tulianzisha kitalu cha miti kupitia fedha zetu za ndani”. amesema Mkurugenzi Rosemary

“Leo tumekutana hapa baada ya kupokea maombi ya micha ya miti ambapo Compass Tanzania imeandaa kitalu cha miti takribani 500 hapa Tinde na Tabora manispaa, kitalu hiki kina thamani ya Tzs 2,500,000. Kwa maombi tuliyopokea kwa awamu hii ya kwanza tunatarajia kugawa miti 400 yenye thamani ya Tsh, 400,000. zoezi hili litaendelea mpaka kufikia malengo yaliyokusudiwa”.

“Miti tunayoigawa leo ni aina ya mitiki (white teek) miti hii inatumika kuzalisha mbao nyeupe yenye thamani kubwa hapa Tanzania na nje ya nchi mithili ya mti pendwa wa Mninga. Miti hii hustahimili ukame na hutoa mazao makubwa baada ya miaka 8-10 inastahili kuvunywa, miti hii pia hutoa kivuli na kuni kwa mahitaji ya nyumbani pia tuna mti wa mlonge ambao hutumika kama dawa tiba mbadala na hutoa kuni na kuhifadhi mazingira kwa ujumla”. amesema Mkurugenzi Rosemary

“Tunaomba Serikali itambue jitihada hizi za shirika letu na kutuweka kwenye kanzi data yake ndani ya Mkoa wa Shinyanga na kutushirikisha pale inapowekekana katika shughuli mbalimbali za ki maendeleo”.

“Tunakaribisha taasisi kubwa za kimaendeleo zinazotoa zuzuku katika maeneo ya utunzaji wa mazingira na haki za binadamu kushirikiana na Compass Tanzania ili kuendeleza kazi hii”. amesema Mkurugenzi Rosemary

Akizungumza meneja miradi wa shirika la Composs Bwana Boniface Mhana amesema shirika hilo linatekeleza mradi  wa kutunza  mazingira katika kata ya Tinde

Mgeni rasmi katika zoezi la upandaji na ugawaji miche ya miti ni kaimu mkuu wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bwana Robet Anatory ambaye amelipongeza shirika la Compass kwa kugawa miche ya miti huku akiwataka wananchi wa kata ya Tinde kuunga mkono juhudi hizo.

Viongozi  mbalimbali waliohudhuria zoezi hilo  wamelipongeza shirika la Compass kwa kugawa miche ya miti huku wakiisihi jamii kuendelea kupanda miti ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikakali.

Meneja miradi wa shirika la Compass Tanzania Bwana Boniface Mhana akitoa elimu ya upandaji miti katika hafla ya kugawa miche ya miti kwa wananchi, shule ya sekondari ya wasichana Tinde, shule  ya Sekondari Kituli, kituo cha afya Tinde, pamoja na Mamlaka ya Mizani kituo cha Tinde.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post