![]() |
Dkt Mrisho Mwacha akimpima Uoni Mwandishi Mwanaidi Bundala |
Na Seif Mangwangi, Arusha
KLINIKI ya macho ya Vision Care imeanza zoezi la kupima Macho Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha ikiwa ni Kuelekea kwenye kilele Cha siku ya Uoni Duniani itakayoadhimishwa Oktoba 12,2023.
Akizungumza wakati wa kuanza zoezi hilo, Mratibu wa zoezi hilo Dkt. Mrisho Mwacha amesema Waandishi wa Habari ni watu muhimu katika nchi hivyo Vision Care imeona ni vyema ikatoa ofa ya Bure kupima Macho Waandishi wa Habari.
Dkt Mwacha amesema kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, zaidi ya Waandishi wa Habari 200 wanatarajiwa kupimwa macho na kupewa ushauri na kuhakikisha wanatekeleza vyema majukumu yao ya kila siku.
![]() |
Waandishi wa Habari kutoka kushoto, Cynthia Mwilolezi-, Vero Mheta na Zulfa Mfinanga wakiwa wamevaa Miwani baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na tatizo la uoni |
" Kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha na katika Kuelekea kwenye kilele Cha siku ya Uoni Duniani, leo 10 Septemba, 2023 tumeanza zoezi la kupima Macho Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha na tunatarajia waandishi wa habari 200 watashiriki zoezi hili,"Amesema.
![]() |
Mwandishi Mwanaidi Bundala akipata matibabu |
Dkt Mwacha amesema tatizo la macho limekuwa likiongezeka miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu nyingi ikiwemo kukua kwa Teknolojia hususani matumizi ya Tv, Kompyuta na Simu na Waandishi wa Habari ndio watumiaji wakubwa hivyo ametoa wito Kwa waandishi kufika kwa wingi ili kujua afya zao.
" Unajua siku hizi Teknolojia imekuwa sana, matumizi ya vyombo vya kielekroniki ni makubwa, tatizo la macho ni kama magonjwa mengine, huwezi kujua mpaka upate vipimo, unaweza kujiona mzima lakini ukija hapa tukagundua una tatizo kubwa ambalo hukuweza kuligundua ,"amesema.
![]() |
Mwandishi wa habari John Mhala akipimwa Uoni, kulia ni Dkt Mrisho Mwacha |
![]() |
Dkt Mrisho Mwacha akimuhudumia John Mhala |