KILOMETA 2.8 ZA MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI UMEJENGWA WILAYANI KARATU

By Ahmed Mahmoud


Wilaya ya Karatu imefanikisha kujenga barabara za kiwango cha lami zenye kilometa 2.8 kati ya mtandao wa barabara wenye kilometa 712 kwa ajili ya kuupendezesha mji huo na kuwa mvuto kwa watalii.

Akiongea mara baada ya kutembelea barabara hizo Mjini Karatu Meneja wa Tarura wilayani ya Karatu Mhandisi Msetu Madara Siku ya mwisho ya Kikao Kazi cha Tarura Mkoa wa Arusha amesema wanashukuru Rais Samia kwa kuleta fedha sanjari na Mkuu wa Wilaya hiyo Dadi Kolimba kusimamia kwa karibu zoezi Zima la Ujenzi huo.

Amesema kwamba kama mnavyojua mji huu ni kitovu cha Utalii tunataka upendeze na vilevile tunataka tumuunge mkono Mh Rais Dkt.Samia baada ya ile filamu ya The Royal tour ambayo kimsingi kwa sisi tulio kwenye lango Utalii kuelekea kwenye vivutio natumeona wamefurika hivyo lazima tuboreshe miundombinu ya barabara ili wakija waweze kufurahia.

Aidha Mhandisi Madara amesema ili kuongeza mtandao huo kuona Mh. Rais alivyofanya kwa Tarura wilayani humo kwa Leo tumetembelea kuona km 2.2 za lami ambazo zimejengwa katika kipindi kifupi cha awamu ya Sita, lakini pia tunaendelea na ujenzi wa madaraja, makaravati,vivuko, katika maeneo korofi wilaya nzima kwa ujumla Hadi Sasa tumefanikiwa.

Kwa mujibu wa Mhandisi Madara amebainisha kwamba baada ya Ukaguzi wao waneweza kubaini makaravati 296 na madaraja 21 ambayo tumeweza kuyajenga  kwa nyakati tofauti kwa mfano tunalo daraja Kubwa lenye upana mita 7 ambalo limeondoa adha kwa wananchi wa eneo la Endamariek

Hata hivyo tumeweza kujenga madaraja mbalimbali kwa siku za karibuni eneo la njiapanda Tutsi kwa kutumia Teknolojia ya mawe na kutumia takribani million 32 na eneo la Marera Kilimatembo pamoja na eneo la Sabasaba Mbulumbulu ambapo madaraja hayo ni gharama nafuu na imara sana na yanawasaidia wananchi.

Vilevile tunaendelea kutumia Teknolojia hiyo katika kuhakikisha kwamba tunaboresha maeneo ambayo yana changamoto ya vivuko ili wananchi wetu waweze kupata huduma stahiki lakini pia kama mnavyoona tumeshapata taarifa za uwepo mvua za El nino ambao kimsingi tumeshajiandaa.

Amesema maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Dadi Kolimba na Mkoa John Mongela tunayafanyia kazi kwa kuhakikisha mitaro inapitisha maji vizuri lakini pia kuangalia madaraja mbalimbali kama yana changamoto yoyote na kuweza kuchukuwa hatua za haraka kabla ya maafa kutokea tumejipanga vizuri tusaidie serikali na Mh.Rais katika utekelezaji wa majukumu yake katika maeneo haya ambayo tuko kama wataalamu  katika sekta hii ya barabara.

"Kimsingi tumeweza kutumia zaidi ya shilingi billion 2.37 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023  na kiasi hicho hicho cha fedha tunaenda kutekeleza miradi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa hiyo tunaamini sehemu yeyote tutaenda kuitendea vyema na mitaro mingi inapitika japo Kuna baadhi ya wananchi ambao wanaendelea kutupa taka baadhi ya maeneo"

Akatoa wito kwa wananchi wilayani huo kuacha tabia ya kutupa taka katika mitaro hususani baadhi yao katika maeneo yao ya Kazi mbele ya ofisi zao waache nao wataendelea kutoa Elimu na tumeona muitikio wanaelewa tutaendelea kuwalimisha pia na tunaenda vizuri. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post