KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 35 MKAZI WA MTAA WA SANJO KATA YA CHAMAGUHA MANISPAA YA SHINYANGA AJINYONGA HADI KUFA KWA KUTUMIA PAZIA

Baba mzazi

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kijana anayefahamika kwa jina la Mbogo Sospeter mwenye umri wa Miaka 35 mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga amejinyonga hadi kufa kwa kutumia pazia.

Akizungumza Baba mzazi wa kijana huyo, Mzee Sospeter Makula amesema tukio hilo limetokea  Oktoba 21.2023 majira ya saa mbili usiku baada ya kijana huyo kutoka kwenye shughuli zake za kila siku.

Mzee huyo ameeleza kuwa marehemu Mbongo hakuwa na changamoto yoyote ile na kwamba walikuwa wanaishi kwa amani na upendo.

“Majira ya saa mbili usiku alikuja kijana wangu akiwa na bodaboda akaniambia nipe shilingi elfu moja nimlipe huyu bodaboda niliingia ndani nikatoa hela nikampa huyo bodaboda akaondoka baada ya hapo nilimuacha nyumbani mimi nikatoka nikaenda kukaa nyumba ya pili tukani kwa jirani yetu baada ya kurudi nyumbani nilikuta taa ya nje inawaka ila taa ya ndani imezimwa nikaingia ndani kuwasha ile taa nikamkuta motto wangu amejinyonga na tayari ameshakufa nilihangaika kuikata ile kamba badaye nikafata kisu nilipoikata kamba basi nikaondoka kwenye kutoa taarifa kwa majirani”.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha Bwana Moshi Ngoyeji amesema baada ya kupokea taarifa za tukio hilo  alichukua hatua za haraka kutoa taarifa kwa mamlaka nyingine ikiwemo Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema  jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha Bwana Moshi Ngoyeji

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post