JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA KUMNYONGA HADI KUFA MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 85, MKAZI WA KITONGOJI CHA NYAMBUI KATA YA TINDE

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili wanaosadikiwa kuhusika na tuhuma za  kumnyonga hadi kufa Mzee Masanja Tungu Masesa mwenye umri wa Miaka 85, Mkazi wa kitongoji na kijiji cha Nyambui kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyambui  Bwana Masesa Mkata tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  Oktoba 21,2023 katika kijiji cha Nyambui kata ya Tinde.

“Mnamo muda wa saa mbili usiku mzee Masanja alikuwepo tu nyumbani na mjukuu wake baada ya kula chakula cha usiku waliingia ndani kulala kila mtu kwenye chumba chake basi yule kijana badaye alisikia babu yake kama vile anagombana na mtu furani alipoenda alikutana na mwanaume amevaa nguo za kujifunika uso kama vile ninja likamkalipia kwa kumtishia akarudi ndani kulala, baada ya kumaliza mwanaume huyo alichukua unga, mahindi akachukua na godolo likaondoka yule kijana lilimwambia asipige kelele kuja kuangalia asubuhi akakuta yule mzee amenyongwa”.amesema Mwenyekiti Masesa

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amethibitisha kukamatwa kwa  watuhumiwa hao wawili ambao wanadaiwa kuhusika na tukio hilo.

‘Tunaendelea na upelelezi lakini hata hivyo katika upelelezi huu tayari tumewakamata watu wawili lakini bado tunaendelea na uchunguzi  ili kubaini chanzo cha tukio hilo”.amesema kamanda Magomi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post