Ndoa ya Inspekta Ally yawaacha wakazi Arusha Midomo wazi

Inspekta Ally akiwa na Mkewe Bi. Selani Sumai
Inspelta Ally na Bi. Selani 
Inspekta Ally akiwa na Mkewe Bi Selani mara baada ya kufunga ndoa
 Na Pamela Mollel,Arusha 


Inpekta wa Jeshi la polisi Tanzania, Ally Babu amefunga ndoa ya kijeshi na mchumba wake Selani Sumai jijini Arusha na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo viongozi wa Serikali.


Tukio hilo liliweza kuwavutia hisia za wakazi wa Arusha  ambao walijitokeza kushangaa gwaride la kijeshi lilivyofanyika wakati wa kwenda kuoa na baada ya kutoka kuoa nyumbani kwa Bi.harusi na baadae tafrija kubwa kufanyika katika hoteli ya Mt.Meru

Ndio hiyo iliwaacha wakazi wa Arusha midomo wazi hasa kutokana na umaridadi wa askari waliokuwa wakipiga gwaride kwa ustadi wa Hali ya juu.

Kwa kawaida Askari anapooa maafisa wa ngazi yake hushiriki kwenye gwaride maalum ambalo mara nyingi hufanyika katika eneo maalum tofauti na shughuli ya ndoa ya Ally na Bi harusi Selani ambayo ilifanyika katika eneo la wazi.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post