MGODI WA DHAHABU MWAKITOLYO WAJENGA SHULE NA KUKUNUA AMBULENSI KUOKOA MAISHA YA WACHIMBAJI, MAMAWAJAWAZITO NA WATOTO.

Na Elias Gamaya Shinyanga 

Mgodi wa dhahabu Mwakitolyo kitalu namba 5 uliopo halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kwa kutambua mchango wa sekta ya elimu na na kutambua changamoto zinazowakabili wachimbaji, mama wajawazito na watoto umenunua gari abulensi aina ya toyota haisi pamoja na kuwajengea vyumba vitatu vya madarasa, ofisi moja na madawati 135 ili kuchochea maendeleo kwenye kata hiyo.

Akisoma risala kwa mkuu wa wilaya ambae pia ni Mgeni rasim Meneja wa mgodi wa mwakitolyo kitalu No:5 waziri Leonard amesema lengo la kununua gari hilo ni kuwasaidia wachimbaji kuwawaisha hospitali pindi wanapo pata ajari pia mama wajawazito pamoja na watoto.

Leonard amesema gharama za ujenzi wa madarasa hayo, ofisi moja ya waalimu na dawati 135 umeghalimu TSH 68,891, 000 (milioni sitini na nane laki nane na tisini na moja elfu) huku ununuzi wa gari ya wagonjwa ni zaidi ya milioni 60

"kwa takwimu za mwakatana 2022 tumepoteza ndugu zetu wawili kwa sababu ya kukosa usafiri kwa kuwafikisha hospitali hivyo tumeamua kununua gari hili kwa ajili ya kuwawahisha wachimbaji wenzetu hospitali pindi wanapopata shida, sambamba na hilo gali hili pia litakua linabeba wagonjwa wote wa maeneo haya hususani mama wajawazito na watoto ili kuwawahisha hospitali kwani ndio wenye uhitaji mkubwa" amesema Meneja wa mgodi wa mwakitolyo kitalu No:5 waziri Leonard

Kwa upandewake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Mussa Samizi amepongeza jitihada zilizofanywa na wachimbaji hao ambapo kasema"Niwashikuru sana kitalu No:5 kwa kutambua changamito hii kwani unapogusa Afya na elimu umegusa maisha ya mtu mmoja mmoja hivyo niwapongeze sana kwa hatua mliofikia tutaendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega" amesema Samizi

Kwa upande mwingine Samizi amewataka wazazi kupinga vikali juu ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto wetu na kuwataka kukaa makini na watoto dhidi ya wimbi la Ushoga, ubakaji, usanganaji pamoja na ulawiti unaoendelea na kusema

"Wazazi tuwe makini na watoto wetu juu ya mmomonyoko wa maadili sikuhizi kunawimbi kuwa la ulawiti ushoga ubakaji, na ninyi watoto msiwaluhusu mtu yyte akawagusa sehemu zenu za siri akitaka kukugusa mwambie DON'T TOUCH HAPA NI KWANGU, toeni taarifa kwa wazazi wenu,, Mwenyekiti wa kitongoji au kwa diwani ili hatua zichukuliwe"amesema Samizi.

Kwa upande wao wachimbaji wadogo mgodi wa Mwakitolyo No:5 wameeleza namna ambavyo walikua wanapata shida pindi wanapopata ajari mgodini na kusema gari hilo litawasaidia kuokoa maisha yao

 "Sisi kugologosha duarani ni kawaida tu tunapokua humu mgodini, kunawatu wanagologosha na tunawatoa nje wakiwa bado hai lakini usafiri unakosekana wa kuwapeleka hospitali sababu hospitali zipo mbali Shinyanga mjini au Kahama hivyo wanafariki hapahapa tukiwanao ila kwa hilo gari litawapeleka haraka ili wapate matibabu" amesema Henry Kilola mchimbaji

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post