MAJALIWA ATOA MAAGIZO KWA WATENDAJI SERIKALI I MKOA WA SIMIYU

 


Na Zurufa Khalfani, Bariadi

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watumishi na watendaji wote wa serikali kuhakikisha wanasimamia vyema miradi yote ya serikali inayotekelezwa katika maeneo yao ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaoendana na thamani iliyotumika.

Akizungumza wakati wa kikao cha watumishi kutoka idara mbalimbali mkoani Simiyu kilichofanyika mjini Bariadi Waziri mkuu Majaliwa ameagiza usimamizi wa karibu wa miradi yote ya serikali kwa kufuata miongozo ambayo iko katika ilani ya ccm

‘’Wakurugenzi watendaji wana vitabu vya ilani ambayo vina miradi yote ya idara husika ,hivyo nawaomba mfanye katika kwa kufuata miogozo alisema kassim majaliwa .

Akizungumza katika kikao hicho naibu Waziri Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange amesema serikali inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma pamoja na kupeleka watumishi katika maeneo yenye upungufu.

Awali akizungumza katika kikao hicho mkuu wa mkoa huo Dk. Yahaya Nawanda amesema katika utatuzi wa migogoro hasa ya ardhi wamefanikiwa kutatua migogoro jumla ya 172kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya na hivyo kuleta amani kwa wananchi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post