VIONGOZI KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI NCHINI WATAKIWA KUJITATHMINI

Rais wa klabu za waandishi wa habari Nchini (UTPC),  Deo Nsokolo akizungumza na viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga 

Na Seif Mangwangi, Morogoro

VIONGOZI wa klabu za waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanyia mabadiliko ya Uongozi  klabu zao ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea kufanywa na sekretarieti ya Muunganiko wa umoja wa klabu hizo nchini (UTPC).


Akizungumza na viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi na usimamizi wa fedha Mkoani hapa, Rais wa Klabu za waandishi wa habari nchini Deo Nsokolo amesema bila kufanyia mabadiliko ya Uongozi kuna baadhi ya klabu zitanyimwa fedha za kujiendesha.

Viongozi wa klabu za waandishi wa habari kutoka Mikoa ya kanda ya Kaskazini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mtoa mada (hayuko pichani)
Mwezeshaji Nice Lema akiwasilisha moja ya mada ya matumizi bora ya fedha katika mafunzo kuhusu utunzaji wa fedha na utawala yanayoendelea Mkoani Morogoro

Amesema moja ya mabadiliko yanayotakiwa kufanywa na klabu za waandishi wa habari ni pamoja na kuhamasisha waandishi wengi zaidi wanajiunga uanachama katika klabu zao ili kuboresha umoja wa waandishi nchini.


“Tunataka mabadiliko makubwa yafanyike katika siku za usoni, mmeletwa hapa kwa ajili ya kukumbushwa majukumu yenu katika Uongozi na lengo kuu tunalotaka ni kuboresha waandishi wetu lakini tutaboresha hali zao wakiwa ndani ya vyama vyetu,”amesema.


Nsokolo amesema moja ya mkakati wa kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka ni kuangalia masharti ya kujiunga ili kuyafanyia marekebisho iwapo yataonekana magumu “uhai wa chama ni wanachama, inasikitisha kuona klabu ina wanachama ishirini wakati waandishi wa habari waliopo nje ya klabu ni zaidi ya Hamsini, nashauri nendeni mkaangalie mashrti yenu kama ni magumu myarekebishe”.


Amesema kwa sasa UTPC imebadili utaratibu wa utoaji wa fedha kwa klabu kwamba klabu itapewa fedha kulingana na idadi ya wanachama “Hivi kweli ni sahihi tutoe kiwango cha fedha sawa kwa klabu zote wakati kuna klabu zina wanachama 20 na nyingine zina wanachama 90?, hii haliwezekani kabisa, mbadilike ili muende sawa na kasi ya UTPC” alisema Nsokolo


Nsokolo amesema viongozi wanapaswa kuwa wamoja na wawazi kwa kila taarifa inayohusu klabu ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima ambayo imekuwa ikififisha maendeleo ya klabu nyingi za waandishi wa habari nchini.


Awali akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Arusha ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya UTPC, Claud Gwandu aliwataka viongozi wa klabu kufuatilia mafunzo hayo kwa makini ili kuivusha UTPC kutoka bora na kuwa bora zaidi.

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Arusha Claud Gwandu akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya fedha na utawala kwa viongozi wa klabu za waandishi wa habari katika mikoa ya kanda ya kaskazini 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post