Shirecu waishukuru Serikali ya Samia

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU kimeishukuru serikali kwa kusimamia hatua ya upandaji wa bei ya pamba kutoka 1550 hadi kufikia Sh. 2000 kwa kilo moja.


Akizungumza na Mwandishi wetu makamu Mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga bwana Joseph Limbe amesema bei inayopaswa kutumika kununua zao la pamba kilo moja ni shilingi 2000 ambapo kabla ya bei hiyo kilo moja ilikuwa ni 1550.


''Tarehe 25 Mwezi wa Nne tulikaa na kutathmini bei ambayo mkulima Mwaka huu ataanza nayo moja kati ya vitu ambavyo viliweza kuzungumziwa zaidi ilikuwa ni kutoa kipaumbele kwa bei ambayo imfikia mkulima ambayo bei elekezi tuliyoanza nayo ilikuwa Elfu moja miatano na hamsini lakini mpaka leo hii katika Mkoa wa Shinyanga bei imefika Shilingi Elfu mbili, kwahiyo serikali yetu imeweza kuliona hili na imeratibu vizuri''. amesema Limbe


Makamu mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Limbe ameipongeza serikali kwa kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto za mazao ya wakulima huku akiiomba kurudisha mfumo wa stakabidhi gharani ili kutoa fursa mbalimbali.


Limbe amesema baada ya msimu wa zao la pamba kuna msimu  wa mazao mengine ikiwemo Dengu na Chorolo ambapo ameiomba  serikali kuendelea kutafuta masomo nje ya Nchi ili msimu ukifika mazao yasafirishwe bila changamoto ambapo pia itakuwa ni fursa kwa mkulima.  


Amesema Machi 28, Mwaka huu 2022 ulifanyika mkutano mkuu wa kwanza tangu bodi hiyo iwepo madarakani ambapo wanachama wa chama cha ushirika Mkoa wa Shinyanga walitoa ushauri na kuagiza kutatuliwa kwa changamoto ambazo zilikuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya chama hicho.


Makamu Mwenyekiti Limbe amesema bodi hiyo inaendeleo vizuri katika kutekeleza maagizo ya wanachama na wadau mbalimbali ambayo waliazimia  ikiwemo kufufua jineri ya mhuze pamoja na kufuatilia viwanja vyenye changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya hati.


Amewaomba wanachi, viongozi na serikali kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa chama hicho pale kinapohitaji msaada ili kutatua changamoto zote zinazokwamisha maendeleo na kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post