DED Shinyanga awahakikishia wananchi wake maisha bora

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomary Satura amesema ataendelea kusimamia kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ili kuinua uchumi wa Manispaa hiyo.


Ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum ambapo pamoja na mambo mengine  amesema Halmashauri hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha inaboresha maisha ya wananchi kupitia huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya, maji, umeme pamoja na miundombinu.


Amesema jitihada zinaendelea za kuhakikisha yanafikiwa maeneo ambayo ni korofi na ni kero kwa wananchi na kwamba mpango wa Halmashauri hiyo ni kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali yakiwemo masuala ya kilimo, ufugaji pamoja na biashara.


Amesema msingi wa kwanza wa utawala bora ni ushirikishwaji wa jamii kwenye kufanya maamuzi ambapo amefafanua kuwa ni wajibu wao kuendelea kushirikiana na wananchi katika uwekezaji pamoja na masuala ya kiuchumi ndani ya Manispaa ili uweze kukua na kuleta maendeleo.


Mkurugenzi Satura amewaagiza viongozi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwashirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo ili kuondoa migogoro.


''Ninafanyia kazi mambo mbalimbali ambayo wananchi wameyaibua wao wenyewe kupitia mikutano yao na badae yakawasilishwa kwenye Halmashauri kwa namna mbalimbali kama Mwenyekiti wa eneo husika anawanyika haki wananchi wake ya kushiriki kwenye shughuli za kujiletea maendeleo siyo sahihi hata kidogo na kiongozi wa namna hiyo hata Taifa hili za Tanzania halimhitaji haya ndiyo mambo ambayo yanaturudisha nyuma katika maendeleo hakuna nmna yoyote sisi tunaweza kufikia maendeleo bila kuwashirikisha wananchi''


 ''Anapotokea kiongozi mmoja anashindwa kuishirikisha jamii katika shughuli za maendeleo halafu anafanya mambo mengi kiusiri yeye peke yake anazusha hoja zingine nyingi kwamba usiri huo unatokana na nini na ndiyo maana wakati mwingine watu wanadhani kwamba kunaubadhirifu na mambo mengine yasiyofaa kwa sababu ya usiri usiokuwa na haja ya namna yoyote naomba nitumie fursa hii kuahidi kwamba hili tutalifanyia kazi''.amesema Satura


Satura pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kuendeleo kutoa ushirikiano kwenye suala ya usafi wa mazingira ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.


 Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeweka mikakati ya kuendelea kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani.


Aidha mkurugenzi huyo amezungumzia suala ya machinjio ya kisasa ambayo ipo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, amewatoa wasiwasi kuwa machinjia hiyo iko salama na inaendelea vizuri ambapo amesema changamoto iliyopo kwa sasa machinjio hiyo inachinja chini ya kiwango kwa sababu ya mahitaji madogo kwa wananchi.


Machinjio ya kisasa iliyopo kata ya Ndembezi inauwezo wa kuchinja Ng'ombe taklibani 500 na mbuzi 1000 kwa siku moja ambapo Satura amesema wanaendelea kutafuta masoko katika maeneo mengine ili kufikia malengo ya machinjio hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post