Mwalimu wa Madrasa Mbaroni akidaiwa kulawiti wanafunzi 22, mmoja akutwa na Maambukizi ya HIV

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha Saidi Mtanda ameamuru kufungwa kwa madrasa iliyopo Kata ya Terati jijini Arusha inayomilikiwa na Mzee Jumanne Ikungi.


Mtanda amechukua uamuzi huo mbele ya kikao cha wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi mkonoo mara baada ya kuwepo kwa taarifa za wanafunzi 22 wanaosoma katika shule hiyo kulawitiwa na mtu anaetuhumiwa kuwafanyia ukatili huo watoto hao ni mzee Jumanne ambae ni mwalimu na Mmiliki wa Madrasa hiyo.


Akiongea mbele ya Kikao hicho Mkuu wa Hule hiyo mwalimu LUCIAN NICHOLAUS MANIMO alimueleza mkuu wa wilaya na wazazi kuwa walibaini tatizo hilo la wanafunzi kufanyiwa ukatili wa kijinsia kutokana na utoro wao na walipo wabana kuwahoji ndipo wakaeleza kuwa huwa wanafungiwa ndani ya nyumba ya mzee Jumanne wakienda madrasa.


Diwani wa Kata hiyo Julius Lenina Meori nae alieleza katika hatua walizozichukua za kuwapima watoto hao 22 tisa wameharibika vibaya kutokana na kulawitiwa huku mmoja vipimo vya Afya vimeonyesha ameshaambukizwa virusi vya Ukimwi.


Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya mh Saidi Mtanda aliwaeleza wazazi hao kuwa jukumu la kulea na kuwalinda ni la walimu na wazazi na jamii na kushangaa kwanini jamii ilifumbia macho swala hilo ambalo yeye alieleza kuwa aliweka mtego zaidi ya wiki Moja ili kumnasa Mzee Jumanne lakini alivyoona watoto wanaendelea haribika akaamua wakapimwe watoto na ilipobainika ni kweli wamelawitiwa ndipo akaliagiza jeshi la Polisi limkamate kutumiwa huyo.


Baada ya kumaliza kikao na wazazi mh Matanda alitoa Agizo kwa wakuu wa Idara ya Elimu na Afya wakishirikiana na Maafisa Ustawi wa jamii kuweka utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa jiji la Arusha msingi na Sekondari ili kuwabaini walio fanyiwa ukatili wa kulawitiwa na kubakwa ili waweze kukomesha vitendo hivyo. 


Mtanda pia alizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Mkono na Shule ya Sekondari mkono kisha wakamwandikia kwa siri majina ya watu wanaowafanyia vitendo vya ukatili huku jina la mzee Jumanne likijirudia mara nyingi katika majina hayo.


Baada ya hapo Mtanda alifika katika Madrasa hiyo na kuifunga kwa kusema kuwa kwakuwa inakabiliwana tuhuma mafundisho katika Madrasa hiyo yasitishwe kwanza huku akionya mtuhumiwa asiachiwe na kuonya rushwa isitumieka kumtoa polisi hadi afikishwe mahakamani Ili sheria ikaamue kama anahatia au vinginevyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post