Kamati ya Bunge yatinga Tume ya mionzi

 

Picha ya pamoja ni Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kufanya ziara katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa
Wakwanza kulia ni Amosi Nungu Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Aliyeshika kipaza sauti ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya jamii Aloyce John Kamamba 
Mkurugenzi mkuu wa Teknolojia na huduma za kiufundi TAEC Dkt.Remijius Ambrose Kawala akiongoza msafara wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na wakionyeshwa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa maabara hizo
Mkurugenzi mkuu wa Teknolojia na huduma za kiufundi TAEC Dkt.Remijius Ambrose Kawala akiwa na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na wakionyeshwa namna mradi huo ulivyoanza  katika na kuangalia utekelezaji wa mradi na.6352 Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, hadi sasa umekamilika kwa 94%

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE HUDUMA NA MAENDELEO YA WATEMBELEA (TAEC) KUONA MRADI WA MAABARA TENGAMANO AMBAO UMEKAMILIKA KWA 94%

Na Vero Ignatus,Arusha

 Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na imefanya ziara katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, na kuangalia utekelezaji wa mradi na.6352 kuhusu ujenzi wa maabara tengamano, ambayo iliingia mkataba na (TBA) kwaajili ya ujenzi huo awamu ya kwanza uliokuwa na kiasi cha fedha bilioni 2.3 hadi kukamilika kwake

Akisoma taarifa ya utekelezaji huo leo katika makao makuu ya TAEC mkoani Arusha Mkurugenzi mkuu wa Prof.Lazaro Busagala amesema kuwa, ujenzi huo ulihusisha maabara kupima viali kwenye sampuli,viwango vya mionzi kwa wafanyakazi kwenye mazingira ya mionzi,uhakiki wa vifaa vya kukagua mionzi,kupima vyanzo vya ionzi kenye mwili wa binadamu,pamoja na kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi.

Prof. Busagala alisema kuwa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara TAEC iliingia mkataba na Li Jun Development Construction CO.LTD 2019 mkataba wa miaka 3, ambapo una thamani ya bil.10.4,na kusema kuwa ujenzi  rasmi changamano ulianza 23sep 2019,hadi kufikia 09 machi 2022 ujenzi huo ulikuwa umefikia 94%ambapo upo mbele kwa miezi mitatu

''Ujenzi huo unahusisha maabara ya kupima mionzi ya alfa ,kupima mionzi Beta,ya kupimia mionzi ya Gama ,kupima mionzi ya kwenye damu,viwango vya metali kwenye sampuli,kutengeneza vifaa vya mionzi ,uandaaji wa sampuli na kemikali,pamoja na maabaa ya kufanyia matengenezo ya vyanzo vya mionzi  na uchunguzi wa nyuklia.

Akichangia katika majadiliano baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya jamii Aloyce John Kamamba ,ameipongeza  TAEC kwa kutekeleza mradi huo kwani ni mzuri na unaridhisha na pesa zimetenda kazi iliyokusudiwa

Kamamba ameishauri Tume hiyo kupitia Katibu wa kamati ya kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya Jamii, kuandaa muda wa kutosha ili wabunge waweze kufahamu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, pamoja na changamoto zinazowakabili kwani taarifa zinaonyesha kuwa hadi sasa vipo vituo 1200 ila kwa mwaka ni vituo 650 tu vinafikiwa 

Nae Mjumbe wa Kamati hiyo Mbunge wa Vyuo Vikuu Dkt.Pauline Nahato amesema kuwa tume hiyo imeanzishwa mwaka 2003 ,ila yeye leo ndio anaifahamu hivyo,amesema ipo haja ya wao kuhakikisha kuwa wanaitangaza ili watu waifahamu, pamoja na utendaji kazi wake  kwani ni wazi kuwa haifahamiki kwa watu wengi

''2003 nilikuwa mbali sana unaweza kuona mimi leo ni kingozi na ndio naifahamu Tume tena kwa uchache jamani,hebu wekeni mpango mkakati wa kujitangaza ili jamii na Taasisi mbalimbali ziwafahamu kwani utendaji kazi wenu ni mkubwa ila hamfahamiki jamani''alisema Nahato

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum kutoka Lindi Tekla Ungele alisema kuwa kwa upande wa kusini mwa nchi kuna mabaki ya vyuma vya silaha za kivita ambayo yalikuwa yanatumiwa na wapigania uhuru wa nchi,hivyo ameiomba TAEC kufanya mchakato wa kuweza kwenda kuviondoa kwani vinaonekana ili visilete madhara kwa wananchi 

Bila shaka kwenye hizo zana zilizokuwa zinatumika kwaajili ya kupigania uhuru sidhani kama hakuna vyenye mionzi,hivyo basi tunaiomba tume ipange mkakati wa kwenda na kuona namna ambayo inaweza kuviondoa au namna ambayo wanijua wao isijeleta madhara kwa jamii''alisema Ungele

Nae Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameishukuru kwa dhati Kamati ya kudumu ya Bunge na Maendeleo ya Jamii ,kwa kutembelea katika Tume ya Nguvu za Atomiki na kujionea kile kinachoendelea  pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Mkenda amesema ni matarajio ya Taasisi kuwa serikali itaendelea kuiwezesha kufikia malengo yake kwa manufaa ya jamii ya  watanzania  

Tume ya Nguvu za Atomic Tanzania inatekeleza majukumu yake chini ya wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ,ilianzishwa 2003 kwa sheria no 7 ,lengo la kuanzishwa ni kusimamia,kudhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia nchini,kulinda afya ya wafanyakazi,wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

Nae Mbunge kutoka Mwanakwerekwe Kasim Hassan Haji ameishauri wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia kupitia waziri Prof.Adolf Mkenda kuangalia katika mitaala ya wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu namna ambayo wanaweza kuweka somo la matumizi sahihi ya mionzi na madhara yake ili waweze kuifahamu kwa upana zaidi

''Nasema hivyo kwasababau ni kweli Tume hii ya inafanya kazi kubwa ni vyema jamii ikaifahamu kwa mapana zaidi hivyo jikiteni pia kwa kutumia vyombo vya habari zaidi na kualika taasisi mbalimbali kuja kuwatembelea mtajenga wigo mpana zaidi''Alisema Haji

Mwisho

 
Reply Forward

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post