BODI YA TMDA YAVAMIA MPAKA WA NAMANGA, YAPOKEA TAARIFA YA UKAGUZI MPAKANI

 

Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, kushoto ni mwenyekiti wa Eric Shitindi,Mkurugenzi Mkuu TMDA,Adam Fimbo,Prof.Appolinary Kamuhabwa na Prof.Said Aboud akifuatiwa katibu Tawala mkoa wa Arusha Athuman Kihamia, kabla ya kuanza safari kuelekea Mpaka wa Namanga kwaajili ya kuangalia utendaji kazi .

      Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,mwenyekiti wa Bodi TMDA Eric Shitindi,akifuatiwa na Mkurugenzi  Mkuu wa TMDA Adam Mitangu Fimbo,wa kwanza kushoto ni Prof.Said Aboud mjumbe wa Bodi,pamoja na Prof.Appolinary Kamuhabwa mjumbe wakikagagua nyumba ya Mamlaka hiyo iliyopo mpakani Namanga

Muonekano wa mpaka wa Namanga wilayani Longido Mkoani Arusha
Mkurugenzi Mkuu TMDA Adam Mitangu Fimbo Akiwa katika Forodha ya Namanga

Paul Mali Kamkulu (TRA)Meneja Msaidizi Forodha,Ushirikiano kati yetu  na taasisi nyingine za serikali ,tunashirikiana vizuri kuhakikisha kwamba kinachoingia kinakuwa kimepata kibali kutoka TMDA
Mrakibu Msaidizi Frank Lubilo ,Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,walipotembelea Forodha hiyo ya Namanga kuona utendaji kazi unavyoendelea
 Mkurugenzi mkuu TMDA Akiwa na Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiangalia dawa zilizofanyiwa ukaguzi tayari kupelekwa maabara hamishika (Minilab Kit) ili kuhakiki ubora wake,forodha ya Namanga Mkoani Arusha.
Kamati ya Ziara ya waumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA,wakiwa katika chumba Cha baridi Cha kuhifadhiwa dawa katika forodha ya Namanga Mkoani Arusha

Meneja wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick mwenye (tshirt nyeupe),wa tatu kutoka kushoto (mwenye shati la draft ni Meneja wa huduma za Kisheria TMDA Iskari Fute,wakiwa wamesimama kwenye nyumba ambayo inatumika kwaajili usimamizi wa shughuli za forodha za Namanga

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) katika kuhakikisha kuwa inadhibiti uingizaji wa bidhaa holela nchini ,Kuanzia julai 2019-januari 2022 jumla ya  magari 3534 yalikaguliwa katika kituo Forodha Namanga ,ili kujiridhisha kuwa magari hayo hayajabeba dawa ambazo hazina vibali vya Mamlaka hiyo.

Aidha katika kuanzia  Julai, 2019 – Januari, 2022 Jumla ya mizigo 1,508 (dawa 1,216 na vifaa tiba 292) ilikaguliwa kwa ajili ya kuingizwa nchini na mizigo 605 (dawa 69 na vifaa tiba 536) ilikaguliwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kuanzia Julai, 2019 hadi Januari 2022; baada ya kukidhi matakwa ya kisheria.
 
Akizungumza katika ziara ya wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA, katika mpaka wa Namanga Mkoani Arusha, Mwenyekiti wa bodi hiyo  Eric Shitindi ,alisema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kuangalia utendaji kazi unavyoendelea,kujua changamoto na namna ya kuzitatua.
 
Mara baada ya ziara hiyo Shitindi alisema kuwa, wameridhishwa na taasisi zote za serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaouonyesha kwa kufanya kazi kwa pamoja,hivyo basi kulingana na taarifa waliyoipokea kituoni hapo inaonyesha kuwa ,bado wanahitaji kuongeza idadi ya watumishi, kwani kwa sasa wapo 3 na eneo hilo linafanya kazi masaa 24 kwa siku 7.

''Kwakweli ukilinganisha na sehemu nyingine ambazo tumepita tumefurahishwa sana jinsi ambavyo tunavyotekeleza majukumuyetu Namanga, kwani mpaka huu ni mkubwa  ambao unaingiza bidhaa nyingi hususani za dawa, wakaguzi tunao ambao wanafanya kazi yao vizuri ,pia mamlaka hapa zimetupa ofisi nzuri ya kuhifadhi dawa zile ambazo zinaingia bila utaratibu,lakini bado kunauhitaji wa watumishi''  alisema Mwenyekiti Shitindi.

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba( TMDA) Adam Mitangu Fimbo,alisema kazi yao kubwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinakuwa salama, bora, fanisi na kulinda afya ya jamii, hivyo katika kutekeleza majukumu wanao mfumo wa kufanya ukaguzi ,mfumo wa kutoa vibali vya kuingia na kutoka nje ya nchi, ambapo katika vituo mbalimbali vya forodha wanakagua bidhaa zote zinazo ingia na kutoka,na kuhakikisha kuwa zinakidhi matakwa ya kisheria
 
''Bidhaa kwa mfano zinazoingia nchini zinatakiwa ziwe bora salama na fanisi na zisiweze kuleta athari zozote kwa mtumiaji,wakaguzi wanafanya kazi hiyo masaa 24 kuhakikisha kuwa nchi hii inalindwa hatuingizi bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu kama vile dawa bandia,dawa duni ,ambazo hazijasajiliwa tunazitafuta kwasababu haziruhusiwi kuingia nchini na kuwa na kibali maalum cha TMDA''Alisema Fimbo

Fimbo alisema kuwa katika ziara hiyo ya bodi waliweza kupita katika mipaka ya Horohoro,Bandari Tanga,Holili,Tarakea mkoani Klimanjaro,na Namanga,ambapo waliweza kuzungumza na watendaji katika  forodha hizo na kugundua changamoto kubwa ni  kutokuwepo kwa scanner katika vituo vyote walivyopita.

Hivyo basi kwa kutambua changamoto hiyo TMDA,wameiomba  TRA kuweka SCANNER ili kusaidia kubaini uwepo wa dawa katika  makontena au magari,ili iweze kuwa raisi kugundua wale ambao wanaingiza bidhaa za dawa bila kufuata taratibu,waweze kuzizuia zisiingie nchini na kuweza kuleta athari kwa binadamu  
 
Amesema kwa hali ilivyo sasa, dawa bandia nchini ni kama 3% na hiyo inaashiria kwamba siyo asilimia kubwa kwani wameweka mifumo mizuri inayofanyakazi, kudhibiti bidhaa kabla hazijaingia ndani ya nchi,hivyo hali siyo mbaya nchini ukilinganisha na nchi nyingine.
 
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick alisema kuwa,Mamlaka hiyo inachukua sampuli na kufuatilia Usalama wa dawa, vifaa Tiba na chanjo hususani chanjo za UVIKO 19, pamoja na kukagua na kusajili viwanda na majengo ya kuuzia bidhaa zinazoodhibitiwa na Mamlaka hiyo.

Proches alisema maabara iliyopo Namanga  imeshafanya uchunguzi wa sampuli 173 za dawa za binadamu zilizoingizwa kutoka nje ya nchi, na sampuli zote zilifaulu na kuruhusiwa kuingizwa nchini,hivyo TMDA inaendelea  na zoezi la kuondoa kwenye soko bidhaa zisizofaa kwa matumizi,kutoa Elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa vifaa Tiba,vitendanishi na vupukusi.

Akielezea changamoto zilizopo ,alisema  baadhi ya wafanyabiashara huingiza  bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi pasipo kuzingatia matakwa ya Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura ya 219 na kutoa visingizio kuwa mizigo hiyo ililetwa Tanzania kimakosa.

Mafanikio kuwa ni pamoja na kupata Ofisi rasmi ya TMDA pamoja na vitendea kazi na hivyo kuboresha utendaji kazi katika mpaka huo, chumba kingine maalum kinachotumika kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli za dawa za binadamu kwa kutumia maabara hamishika (Minilab. Kuanzia Julai, 2019 hadi Januari, 2022

 Paul Mali Kamkulu (TRA)Idara ya Forodha na Ushuru,alisema kuwa Ushirikiano kati wao  na taasisi nyingine za serikali ,wanashirikiana vizuri kuhakikisha kwamba kinachoingia kinakuwa kimepata kibali kutoka TMDA,na kuahakikisha kuwa sheria zote katika maeneo yao ya utendaji kazi zinafuatwa kama inavyohitajika

Ameiomba serikali kuangalia changamoto ya maeneo ya makazi yamekuwa tatizo kwa wafanyakazi tofautitofauti waliopo mpakani,kwani wamejikuta wakipanga nyumba kwenye maeneo ya wateja wao wakati mwingine haohao ndio wanakuwa wanaleta bidhaa ambazo siyo sahihi na zisizohitajika.

Kamkulu amesema kuwa pamoja na hayo wanaendelea kupambana wanahakikisha vitu vyote vinavyoingia vinakuwa katika utaratibu,ila makusanyo kama TRA  waliyoatiwa ,ambapo amesema kuwa hadi sasa wapo 100%

Tunatakiwa kukusanya bil.tano ila hadi sasa tumeshakusanya  tumeshakusanya bil.sita  kwa maana hiyo tutakapofika mwisho wa mwezi tutakusanya zaidi ya hiyo.

 Kwa upande wake  Mfawidhi kutoka TMDA forodha ya Namanga Vedasto Uiso alisema kuwa, kazi kubwa inayofanyika katika kituo hicho ni pamoja na  ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na  kupokea maoni yao kwa kutumia fomu ya Customer Exit questionnaire. 

Pia, kituo hicho hufanya uchunguzi wa sampuli za dawa za binadamu,kwa kutumia maabara hamishika (Minilab Kit) ili kuhakiki ubora wake,kwani forodha hiyo ni moja ya vituo ambavyo vinafanya kaguzi za mizigo kwa upande mmoja tu wa nchi (One Stop Border Post - OSBP) ambapo mizigo inakaguliwa kwa pamoja na wakaguzi wa nchi zote mbili 

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post