WAKURUGENZI WA HOSPITALI NA TAASISI ZA AFYA WATAKIWA KUSIMAMIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

 


Na. Catherine Sungura,WAF-Dodoma


Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, Kanda,Maalumu, Taifa pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya wametakiwa kusimamia vipaumbele vya wizara katika  kuboresha huduma za afya ili kuondoa kero kwa wananchi.


Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi wakati wa kikao kazi cha  tathimnini  ya utoaji wa huduma kwa kipindi cha miezi sita kinachofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma.


Amesema kuwa Taasisi zinaongozwa na Sera, vipaumbele za sekta pamoja na dira ya Taifa ya maendeleo hivyo mpango mkakati wa wizara lazima utekelezeke ili kuweza kutoa huduma bora nay a viwango kwa watanzania.


Prof. Makubi amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwao kwani kinasaidia kujitathimini katika utoaji wa huduma za afya kwa kipindi cha miezi sita iliyopita pamoja na kujipanga kwa miezi sita ijayo ilikujua nini wanapaswa  kufanya  kusaidia hospitali kwa kipindi cha miezi sita.


 “Sasa hivi sekta ya afya ipo katika maboresho makubwa ya miundombinu pamoja na vifaa,hivyo lazima tuunganishe maboresho hayo ili yaweze kuonesha ubora wa huduma pale mgonjwa anapofika aweze kupata huduma zote anazohitaji katika hospitali.


>Ameongeza kuwa tathimini hiyo itawaonesha kwa namna gani wamefanya vizuri na pale ambapo hawakufanya vizuri kwa wananchi waweze kufanya vyema wanapoelekea mwisho wa mwaka wa bajeti ya Serikali.


“Tunategemea wakurugenzi wanaporudi kwenye hospitali zao wakaendelee kuboresha huduma zaidi na kuondoa kero na malalamiko kwa wananchi, kwani Wizara haitegemei kusikia kero kutoka kwenye maeneo yao kwamba mama ameshindwa kupata huduma au amekosa dawa hususani kwenye hospitali ya Kanda na Taifa, lazima mwananchi apate dawa”.Alisisitiza prof. makubi


Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwataka Viongozi wote wa hospitali na taasisi wafanye kazi kwa uadilifu,kujituma  na kwa matokeo na kwa kuliona hilo Wizara imekuja na mfumo wa kuwapima wakurugwnzi hao.“Tunataka viongozi waende kwa matokeo kwani hospitali hizo kubwa wanao uwezo wa kununua dawa,tutawapima kufikia malengo tulowapatia na kama tumewapa kuongeza dawa kwa asilimia 10 hadi 20 hivyo tunataka kuona hilo linafikiwa”.


Kwa upande mwingine Prof. Makubi amezitaka taasisi hizo kuunganisha nguvu katika kampeni shirikishi na harakishi ya uhamasishaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili wananchi waweze kuhamasika kuchanja zaidi ili kufikia malengo waliyojiwekea ambapo hadi sasa wamefikia asilimia 3.3 ya wananchi wamepata chanjo ya UVIKO-19.


Kuhusu matumizi holela ya dawa za ‘Antibiotics’ Prof. Makubi amesema wamelipokea agizo la waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu  kupitia kwa Mfamasia Mkuu wa Serikali wanalifanyia kazi na hivyo wameanza kuliandalia mkakati wa uratibu kuona ni jinsi gani mtu anayehitaji kweli hizo dawa apatiwe kwani ipo miongozo ambayo inasisimia matumizi ya dawa , hata hivyo amewakumbusha wananchi kuacha kutumia dawa kiholela pasipo kuandikiwa na watoa huduma na vile vile kwa wauza dawa wasitoe dawa bila kwa wananchi bila ya kuwa na cheti na kuwataka wafuate miongozo ya dawa.


Katika kikao hicho Katibu Mkuu ameweza kuwapitisha wakurugenzi katika maeneo ya vipaumbele vya wizara takriban kumi ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya,bidhaa za dawa, UVIKO-19, Uongozi, Bima ya afya kwa wote, vifo vya mama na mtoto, Magonjwa ya kuambukiza (NCDs), huduma za kibingwa na bobezi, miundombinu na vifaa, watumishi, tehama na takwimu pamoja na tafiti.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post