Makinda ahimiza utoaji zaidi elimu ya sensa kwa wananchi wote

Na Claud Gwandu, Arusha.

 

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anna Makinda, amehimiza kuimarishwa kwa utoaji wa elimu na uhamasishaji kwa wananchi katika ngazi zote za utawala wa nchi  ili washiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini Agosti mwaka huu.

 

Amesema ili wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa ni muhimu kwa wadau wote, katika ngazi zote kuelewa umuhimu na manufaa ya sensa kwa ajili ya maendeleo yao na nchi yao.

 

 “Sensa hufanyika kwa mujibu wa sheria sura ya 351 na umuhimu wake ni kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu, mahitaji yao na hivyo kuweza kupanga mipango ya maendeleo kwa uhakika zaidi.

 

“Takwimu sahihi za kila mtanzania atakayehesabiwa siku ya sensa zitapatikana katika taarifa mbalimbali zitakazojazwa katika madodoso ya sensa hivyo kila mmoja wetu anapaswa kujitokeza ili ahesabiwe yakiwemo makundi maalum katika jamii,” amesisitiza

 

Kamisaa Makinda ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa wito huo jana na leo alipokutana na Kamati ya Maandalizi ya Sensa ya Mkoa wa Arusha na kisha akatembelea kazi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu katika eneo la Sakina jijini hapa.

 

Aliitaka Kamati hiyo ya Mkoa kushirikisha makundi yote katika jamii wakiwemo viongozi wa kidini, viongozi wa kisiasa, wazee wa kimila,watu  wenye ushawishi katika jamii na wananchi wenye ulemavu ili wote washirikishwe kikamilifu katika sense ya mwaka huu ambayo alisema itakuwa ya aina yake kutokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa.

 

Aidha,alitaka migogoro ya mipaka baina ya vijiji na vijiji,vitongoji na vitongoji ishughulikiwe na kumalizwa haraka ili isije ikavuruga utaratibu wa kuhesabu watu katika maeneo husika.

 

Mapema, akitoa taarifa ya Mkuu wa Mkoa, John Mongela  kuhusu maandalizi ya Sensa ya mwaka huu, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Lyamongi David, alisema zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabu watu limekamilika katika halmashauri sita kati ya saba za mkoa huo.

 

“Zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabu watu katika mkoa wa Arusha lilianza Juni 18, mwaka jana, na hadi Januari 25, mwaka huu limekamiika katika halmashauri sita.Kwa sasa zoezi linaendelea katika Jiji la Arusha na linatarajiwa kukamilika Februari 20,mwaka huu,”alisisitiza Kaimu Katibu Tawala huyo

 

Kaimu Katibu Tawala huyo alielezea changamoto zilizojitokeza kuwa ni pamoja na migogoro ya mipaka ambako baadhi ya vitongoji viwili kujikuta vimesajiliwa katika ardhi moja na baadhi ya vitongoji vilivyopo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha kuingiliana na vitongoji vilivyopo wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

 

”Mheshimiwa Kamisaa, changamoto hizo pamoja na nyingine za kisiasa, uhamaji hasa wa wafugaji kutoka eneo moja kwenda linguine kufuata maji na malisho ya mifugo na miundombinu mibovu inayosababisha huduma zisifike kwa urahisi,inaendelea kushughulikiwa katika ngazi tofauti ili kuhakikisha zoezi la sensa,linafanikiwa kama ilivyopangwa,” anasema Lyamongi

 

Sensa ya mwaka huu ni ya sita tangu Tanzania ilipopata uhuru na mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2012  ambayo ilionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na watu 44,928,923.

 

Sensa ya kwanza nchini ilifanyika mwaka 1967, ikafuatiwa na ya mwaka 1978, kishanya tatau ikafanyika  1988 na kufuatiwa nay a nne mwaka 2002, ya tano ikafanyika mwaka 2012 na ya sita itakuwa ya mwaka huu 2022.

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post