Serikali yashauriwa kuweka mikakati ya kudhibiti vifo vya Mama na Mtoto Shinyanga

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Viongozi na wajumbe mbalimbali wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga RCC wameishauri serikali kuchukua hatua madhubuti na za kimkakati katika kukabiliana na changamoto zinazoikumba jamii hasa katika sekta ya Elimu na Afya.Wametoa ushauri huo wakati wa Kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.Wakieleza kuhusu changamoto hizo wamesema kuwa katika sekta ya Afya kumekuwepo na changamoto ambazo zinapelekea vifo vya mama na watoto hivyo kunahitajika hatua za kukabiliana na changamoto hizo.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewaomba viongozi husika kuzichukua changamoto hizo na kwenda kuzifanyia kazi mapema ili kuleta mapinduzi ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga.Katika kikao hicho katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary amewataka wenyeviti wa mitaa katika Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia pamoja na kufikisha taarifa za matukio ya ukatili sehemu husika na kwa wakati ili kupunguza au kuondoa kabisa ukatili wa kijinsia Mwaka huu 2022 na kwamba amesema hatokubali kuona ukatili unaendelea katika Mkoa wa Shinyanga.Wakati huo huo Wabunge wa majimbo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga wamelitaka shirika la umeme TANESCO Mkoani humo kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya malipo sahihi ya kuunganishiwa huduma ya umeme kwa wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini ili kuondoa  maswali.


Wabunge hao wameyasema hayo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa RCC kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.


Iddi Kassim mbunge wa Msalala, Emmanuel Chelehani mbunge wa Ushetu pamoja na mbunge wa Kahama Jumanne Kishimba wameiomba TANESCO Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha  inatoa majibu sahihi kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme katika maeneo ya mjini na vijijini kwa kuzingatia uhalisia wa maeneo husika.


Wamesema zipo changamoto nyingi zinazowakabili wananchi katika majimbo hayo ikiwemo changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara na kusababisha athari.


Aidha Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo amelitaka TANESCO kufanya upya tathmini ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwenye makazi, taasisi za umma pamoja na makanisa na misikiti.


Kwa upende wake meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga mhandisi Grace Ntungi amesema shirika litashughulikia changamoto zote zilizobainishwa na kwamba tathmini ya utekelezaji wa miradi inapofanyika huwa inahusisha maeneo yote lakini utekelezaji wa kuuganisha huduma unategemea zaidi bajeti iliyopo.


Kikao cha kamati ya Ushauri RCC kilichoketi jana ni kikao cha kwanza kwa Mwaka huu 2022 , na kwamba  ni chombo cha kisheria  kinachotoa ushauri wa utekelezaji wa shughuli za serikali za Mkoa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post